Sunday, August 18

ATE kutoa tuzo ya mwajiri bora Desemba

0


By Ephrahim Bahemu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), kimezindua rasmi tuzo za mwajiri bora 2019, huku kikiongeza vipengele vitatu vinavyohusu uendelezaji bora wa mafunzo, uanagenzi na kujali vitu vya ndani.

Akitangaza kuanza kwa mchakato wa tuzo hizo leo Aprili 29, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk Aggrey Mlimuka amesema vipengele hivyo vimeongezwa kutokana na mapendekezo ya ofisi ya Waziri Mkuu na wadau wengine, hivyo jumla ya vipengele kwa mwaka huu vitakuwa 38.

“Tofauti na mwaka jana ambapo tulikuwa na vipengele 35 mwaka huu tutakuwa na vipengele 38, vilivyoongezeka ni mwajiri bora anayeendeleza mafunzo ya ujuzi kwa wahitimu (internship), mwajiri anayetoa mafunzo ya uanagenzi (apprentiship) na mwajiri anayethamini rasilimali za ndani (local content),” amesema Dk Mlimuka.

Amesema lengo la kuongeza vipengele hivyo ni kuboresha tuzo zenyewe kwa kuongoza ushindani, pia kugusa maeneo maeneo muhimu ambayo yanaleta tija katika ukuzaji na uendelezaji wa rasilimali watu katika eneo la kazi.

Dk Mlimuka ameongeza kuwa kutakuwa na tuzo ya mshindi wa jumla kwa mwajiri bora katika sekta binafsi, sekta ya umma na mashirika yaliyopo nchini.

Maelezo zaidi kuhusu tuzo hizo yanapatikana katika tovuti ya ATE.

Share.

About Author

Leave A Reply