Thursday, August 22

Askofu Shoo: Tuseme ukweli kwa ajiliya nchi, kanisa na watu wengine

0


By Florah Temba,Mwananchi [email protected]

Moshi. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, (KKKT)Dk Fredrick Shoo, amesema duniani leo wapo watu ambao wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kuuficha ukweli, bila kujua kuwa ukweli una asili ya kutofichika.

Shoo ameyasema hayo leo, wakati akuzungumza kwenye ibada ya Pasaka ambapo amesema wakristo  Kama wafuasi wa Yesu wanapaswa kuukumbatia ukweli katika mambo yote.

“Tunaweza kusema tunaipenda nchi yetu, lakini swali, kubwa kwetu ni je tunayo ujasiri wa kujitoa kwelikweli hata kiasi cha kutoogopa vipingamizi na vikwazo vya hatari? alihoji na kuongeza kuwa.

Ujasiri peke yake bila upendo unaotoka moyoni, huzaa ukatili na ujasiri usiokuwa na upendo huzaa hofu, na inapotokea kusimama kwa ajili ya wengine kwa manufaa ya wengine upendo bila ujasiri unabakia kuwa upendo wa mdomoni tu.

“Hata leo baadhi ya Wakristo tunaweza kusema tunampenda Yesu lakini inapokuja saa ya kusimama kama Shahidi wa Kristo, kuitetea familia yako, Kanisa na hata nchi yako unaingia mitini, Wakina mama wale hawakusaliti, walisimama kwelikweli, na upendo wao huu wa dhati,” amesema

Amesema ujasiri wa kujitoa kwa ajili ya wengine na Familia, Kanisa na nchi unahitaji watu kama hawa wenye upendo wenye ujasiri na upendo wa kujitoa kwa ajili ya wengine”

Alisema wakati wa Yesu, Maaskari waliokuwa wakilinda kaburi, walipewa pesa nyingi ili kuuficha ukweli lakini haikuwezekana na leo wapo watu ambao wanajaribu kuwazuia Wakristo kutangaza habari za Yesu na kulizuia kanisa kufanya kazi ya Kitume, bila kujua kuwa tendo hilo ni la Mungu mwenyewe.

“Kulifanyika jitihada nyingi kwa ajili ya kuficha ukweli wa Yesu kufufuka, maaskari walioshuhudia lile tetemeko na kushuhudia Yesu kufufuka walikuwa  na hofu kubwa,  walipewa pesa nyingi na wale wakuu wao, ili eti waseme Yesu hakufufuka bali wanafunzi wake walikuja kumuiba usiku wakiwa wamelala”

“Lakini haikuwezekana kuuficha ukweli huo, habari za kufufuka kwa Yesu zikaenea na tena mbaya zaidi hata habari kwamba wakuu waliwapa pesa wale askari ili wanyamaze nazo zikaenea”

“Yamkini duniani wapo  leo pia watu waovu wanaotumia nguvu nyingi kuuficha ukweli, wanasahau kuwa ukweli una asili ya kutofichika daima, tujifunze kwa wale kina mama waliokwenda Kaburini”

Alisema ukweli na Upendo wa dhati ndiyo uliyowafanya kina mama waliokwenda kaburini wadiriki hata kuhatarisha maisha yao.

“Leo hii tunapoadhimisha sikukuu hii ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo, tujifunze jambo kwa kina mama hawa waliokwenda kaburini, walikuwa na upendo wa kweli, ambao  ni tofauti na upendo wa Kinafiki, upendo wa kweli hutoka moyoni, na hutupa ujasiri, hutupa nguvu ya kufanya mambo yale magumu na hata yale yanayoonekana hayawezekani na ya hatari”

Share.

About Author

Leave A Reply