Tuesday, August 20

Askofu awataka waumini wasikate tamaa

0


By Nazael Mkiramweni, Mwananchi [email protected]

Dodoma.  Askofu wa Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Dodoma, Amon Kinyunyu amewaka Wakristo kutokana tamaa pale wanapokutana na changamoto katika maisha yao badala yake wamuombe Mungu awaonyeshe njia ya kukabiliana nazo.

Askofu Kinyunyu ameyasema hayo leo Aprili 21, 2019 wakati akihubiri kwenye ibada ya Pasaka ya kusherehekea kufufuka Yesu Kristo katika Kanisa la KKKT, Usharika wa Kanisa Kuu Dodoma.

Amesema zipo changamoto nyingi zinazowafanya wanadamu kutofikia malengo, wengine wakiamua kujiua, kukimbia familia zao, kurudi nyuma kiimani, wakidhani kufanya hivyo ndio suluhisho.

“Kila Mkiristo anatakiwa kujiuliza afanye nini juu ya changamoto hizo, ni nani atakayeniondolea changamoto hizi, ukweli ni kwamba suluhisho la kweli lipo kwa Yesu pekee, ukikabiliwa na changamoto katika maisha yako zikabidhi kwa Yesu kwani alikufa kwa ajili yetu, hivyo Bwana atakuonyesha namna ya kukabiliana nazo,” amesema Askofu Kinyunyu.

Amesema Yesu ametimiza ya Mungu ya kuukomboa ulimwengu  na kuwa Pasaka ni ukombozi wa dhambi kutoka utumwani walikokuwa wanatumika wanadamu.

Hata hivyo amewataka Wakristo kuamini kuwa kufufuka kwa Yesu ni sababu ya ishara ya ushindi na kutambua kuwa wanadamu wanapokufaa watafufuka kwa ajili ya kumlaki Bwana mawinguni.

“Kufufuka kwake ni sababu ya kutufanya tuamini kuwa tukifa tutafufuka, tusisikitike juu ya kifo, bali tutambue ni kulala na mwishowe tutafufuka kama alivyofufuka Yesu. Hivyo tunatakiwa kufanya mambo ya kumpendeza Mungu ili tuweze kurithi ufalme wa mbinguni,” amesema.

Share.

About Author

Leave A Reply