Friday, July 19

Arusha United haina mpinzani aisee!

0


By Saddam Sadick

Arusha. Arusha United imeutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha baada ya kuichapa Pamba ya Mwanza mabao 2-1, mechi ya Ligi Daraja la Kwanza.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani tukio kubwa lilikuwa ni waamuzi wa mtanange huo kutolewa nje ya uwanja na Askari Polisi wakiwa katika ulinzi mkali.

Waamuzi hao,  Seleman Likele (Dar es Salam), Efrahim Mkumbu na Said Mkono wote kutoka Tanga waliondolewa kwa staili hiyo kwa sababu ya usalama wao.

Licha ya timu zote kutocheza soka la kuvutia, lakini wenyeji walifanikiwa kubaki na alama tatu muhimu na kujiweka kileleni katika msimamo wa Kundi B, kwa kuwa na pointi 14 .

Mabao ya Arusha United yaliwekwa wavuni na Ally Kabunda dakika ya 21, na Ishala Juma dakika ya 45, huku la kufutia machozi kwa Pamba likiwekwa kimiani na Geofrey Julius dakika ya 65.

Share.

About Author

Leave A Reply