Friday, August 23

Angola yaifunga Nigeria mabao 2-1 ikimaliza mshindi wa tatu Afcon U17 2019

0


By THOMAS NG’ITU

Angola amefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la Afcon, baada ya kuifunga Nigeria 2-1. Magoli ya Angola yalifungwa na Osvald Capemba na Zito Luvumbo huku la Nigeria likifungwa na Wisdom Ubani.

Dakika 45 kipindi cha kwanza timu hizo zilikwenda mapumziko kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1.

Katika mchezo huo timu zote zilikuwa zikicheza kwa kushambuliana huku kila mmoja akitaka kupata goli la kuongoza.

Dakika 2 Zitto Luvumbo alipiga shuti kali na kutoka pembezoni kidogo mwa lango la Nigeria, na kipa wa Nigeria, Sunday Stephen alipoanzisha mpira alikosea na kuangukia mikononi mwa Osvaldo Kapemba wa Angola aliyepiga shuti na kutoka nje.

Nigeria walionekana kukosa mipango ya kuweza kupata bao licha ya kwamba viungo wao walikuwa wepesi katika kutengeneza nafasi.

Angola walikuwa wakimtumia winga wao Zitto katika kupeleka mashambulizi na alionekana kuwasumbua vilivyo wachezaji wa Nigeria.

Dakika 27 Capemba aliifungia goli Angola kwa kichwa baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa David Nzanza. Goli hilo liliwafanya wachezaji wa Nigeria na kuomyesha nia ya kuhitaji goli lakini mabeki wa Angola walionyesha umakininkatika kuzuia

Dakika 29 Nigeria walichomoa goli kupitia kwa Wisdom Ubani baada ya mabeki wa Angola kujichanganya ndani ya dimba na yeye kupiga shuti lililoenda moja kwa moja wavuni.

Goli hilo lilizidisha presha langoni kwa Angola kiasi cha kuwafanya mabeki wake kuwa na kazi zaidi ya kuzuia.

Dakika 42 beki wa Angola, Porfrio Cambila alipewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Mayowa Abayomi.

Katika kipindi cha pili Angola walianza kwa kushambulia na mapema dakika 48 Zito Luvumbo aliifungia bao la pili.

Goli hilo liliwafanya Nigeria wazidi kuonyesha uhodari katika kutafuta nafasi ya kupata goli. Dakika 57 Beki wa Angola, Porfirio Abrantes alionyeshewa kadi ya pili ya njano na kupewa kadi nyekundu baada ya kufanya madhambi kwa mchezaji wa Nigeria, Fawaz Abdullahi. Nigeria walifanya mabadiliko dakika 60 kwa kumtoa Olatomi Olaniyan na kuingia Divine Nwachukwu. Pengo la Abrantes kwa Angola lilionekana hali iyomfanya kocha wa timu hiyo, Pedro Goncalves kufanya mabadiliko dakika 69 kwa kumtoa David Azanza na kuingia Antonio Muanza.

Wakati huo huo Nigeria walifanya mabadiliko ya kumtoa Wisdom Ubani na kuingia Akinkunmi Amoo ambaye tangu alivoingia alionyesha kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji. Amoo katika michezo ya nyuma yote alikuwa akinza lakini katika mchezo huu aliingia akitokea katika benchi.

Nigeria walikuwa wakishambulia lakini hawakuweza kuivuka safu ya ulinzi Angola kutokana na mabeki wake kujipanga vizuri kwenye kuzuia.

Dakika 83 Angola walifanya mabadiliko kwa kumtoa Oscald Capemba na kuingia Francisco Junior,mabadiliko hayo yalikuwa yakionyesha kama mbinu ya mwalimu wao kupoteza muda. Wachezaji wa Nigeria wakiongozwa na Amoo walizidi kupeleka mashambulizi lakini hata hivyo hawakuweza kupata goli la kusawazisha.

Share.

About Author

Leave A Reply