Monday, August 26

Ajib atua Mazembe

0


Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib atajiunga kuwa mchezaji mpya wa TP Mazembe.
Ajib anamaliza mkataba wake wa miaka miwili mwezi ujao unaofikia tamati Juni 30,2019.
Mazembe imewaandikia barua Yanga kuwajulisha kuwa watamchukua Ajib rasmi Julai mosi 2019 na kwamba kama kuna utofauti wowote wa taarifa hiyo Yanga iwasiliane nao kwa mujibu wa Kanuni za Usajili za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Katika dili hilo Yanga ni wazi haitapata fedha zozote kutokana na usajili huo kufuatia Ajib kuchukuliwa akiwa amemaliza mkataba lakini pia akimaliza uvumi wa kurejea Simba.
Simba ilikuwa inatajwa kutamani kumrudisha Ajib katika klabu yake ya zamani lakini sasa Mazembe imemaliza rasmi uvumi huo.
Ajib anaweza kuwa mchezaji mapema kusajiliwa na Mazembe baada ya mmiliki wa klabu hiyo Moise Katumbi wiki hii kurejea nchini kwake baada ya kukaa uhamishoni kwa miaka kadhaa huku msimu Mazembe wakifanikiwa kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu nchini DR Congo.

Share.

About Author

Leave A Reply