Wednesday, August 21

Agizo la Magufuli kwa mawaziri

0


By Baraka Samson. Mwananchi

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewaagiza mawaziri wa Tanzania kuitisha kikao cha kamati ya pamoja ya Tanzania na Namibia ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Mei 27, 2019 na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu,  Gerson Msigwa inaeleza kuwa kikao hicho pia kitajadili fursa mbalimbali za ushirikiano wenye manufaa kwa nchi hizo.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo katika mazungumzo kati yake na Rais wa  Namibia, Hage Geingob yaliyofanyika Ikulu ya Windhoek nchini humo.

Rais Magufuli yupo Namibia katika ziara ya kitaifa ya siku mbili.

Ikulu imeeleza kuwa Rais Magufuli alitoa maagizo hayo, baada ya kupokea taarifa kuwa kikao hicho hakijafanyika tangu 1999 na kusababisha masuala mengi yakiwemo ya ushirikiano wa biashara na uwekezaji kutopata msukumo wa kutosha.

Aidha,  amebainisha kuwa licha ya uhusiano wa kihistoria na kindugu kati ya Tanzania na Namibia, ulioasisiwa Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa Nambia Sam Nujoma, nchi hizo zimekuwa na kiwango cha chini cha ushirikiano wa biashara.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa  mwaka uliopita biashara iliyofanyika ilikuwa na thamani ya Sh59.5bilioni,  na  Tanzania kuna kampuni mbili tu za Namibia zinazofanya biashara.

Share.

About Author

Leave A Reply