Wednesday, August 21

TECNO KUJA NA KAMERA YA AINA YAKE

0Kufuatia matoleo ya simu mbalimbali yiliyotangulia, TECNO, imekua ikitajwa tajwa huku ikihusishwa na ujio wa toleo jipya ikikisiwa kuwa ni muendelezo wa matoleo ya Camon, ni ukweli usiopingika kuwa matoleo ya TECNO-Camon yamekua na kamera nzuri zaidi kufananishwa na matoleo mengine

Miongoni mwa vivutizi vinavyoipa simu kipaumbele, bila shaka simu inatakiwa iwe na kamera yenye megapixel kubwa, TECNO, wamelizingatia hilo

Baadhi ya kurasa za mitandaoni zimeihusisha kampuni ya TECNO juu ya ujio wa toleo jipya likipewa jina la Camon kufuatia histoia ya kampuni kuzindua Camon CX mwaka jana miezi kama hii, bado hakujawa na uhakika wa taaifa hizi hivyo ni propaganda tu

Simu hiyo inakadiriwa kuwa na megapixel 16 mbele pamoja na flashi maalum kwa picha za ‘’selfie’’, uwezo wa kupiga picha zenye ubora wa HD, kamera yake ya nyuma kuja na megapixel nyingi zaidi ssambamba na flashi maalum zinaakisi mwanga ili kupata kuendana na mazingira. 

Maswali kuhusiana na ujio wa simu hiyo `yamekua mengi sana pasina kupata majibu yenye uhakika, kamera inayoweza kupiga picha nyingi ndani ya mfupi zikiwa na ubora wa HD?, bado inaniacha na maswali yanayoamsha morali ya kutaka kujua zaidi

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti http//www.tecno-mobile.comRead More

Share.

About Author

Comments are closed.