Saturday, August 17

Walichokisema watu maarufu kuhusu kupigwa risasi kwa mwanafunzi chuo

0


Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), kimethibitishwa kuwa mwanafunzi aliyepigwa risasi hapo jana Ijumaa, Februari 16, 2018 katika eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam na kufariki dunia ni mwanafunzi wa chuo hicho.

mwanafuzni huyo aliyejulikana kwa jina Akwilina Akwiline, ametajwa kuwa ni mwanafunzi wa chuo hicho na alikuwa akisoma shahada ya kwanza ya ununuzi na ugavi.

Ofisa uhusiano wa NIT, Ngasekela David ameeleza kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo, na bado wanaendelea kufuatilia zaidi.

“Ni kweli alikuwa wanafunzi wetu na tumepokea kwa masikitiko taarifa hizi. Tunaendelea kufuatilia zaidi, “amesema David.

Taarifa za kupigwa risasi na kufariki kwa mwanafunzi huyo, zilianza kusambazwa katika mitandao mbali mbali ya kijamii kanzia jana ijumaa Februari 16, na hii leo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Soma hapa Kauli ya polisi kufuatia kupigwa risasi kwa mwanafunzi wa elimu ya juu

Kufuatia kutokea kwa tukio hilo, watu mbalimbali ikiwemo viongozi wa kisiasa na watu wengine maarufu wameeleza kupokea kwa masikiitiko taarifa hiyo huku wengine wakilaani vikali kitendo hicho na kuzitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua stahiki wahusika wote.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo, Twitter, Instagram na Facebook haya ni maoni ya watu mbalimbali kuhusiana na tukio hili.

 

 

 

 

 

Tumbo la uzazi limeniuma jaman 😢😢 R.I.P katoto kazuri kasikokuwa na hatia 🙏🙏

A post shared by Shishi Trump (@shilolekiuno_badgirlshishi) on Feb 17, 2018 at 1:35am PST

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.