Friday, March 22

Usome hapa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa uliowasilishwa bungeni

0


Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni Ijumaa Novemba 16, 2018.

Katika muswada huo miongoni mwa mambo yanayopendekezwa ni kuongezwa kwa kifungu ambacho kitampa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kusitisha usajili wa chama cha siasa kitakachovunja masharti ya sheria husika.

Mbali na jambo hilo, jambo jingine lililojadiliwa katika muswada huo ni kusudio la kuzuia viongozi wa vyama vya siasa kuwa
wajumbe wa bodi ya wadhamini.

Muswada huo unapendekeza pia kuongezwa kwa vifungu ili kuainisha makosa na adhabu na kusitishwa kwa usajili wa vyama vya siasa vitakavyokiuka masharti ya sheria.

Pia, inapendekeza kufanyiwa marekebisho ili kumpa mamlaka waziri mwenye mamlaka ya kutengeneza kanuni za uandaaji wa taarifa za hesabu za vyama vya siasa na mambo yatakayojumuishwa katika katiba za vyama vya siasa.

Hapa chini ni muswada huo, unaweza kuusoma.

Comments

Share.

About Author

Leave A Reply