Thursday, February 21

Safari ya Alphayo Kidata ndani ya miaka mitatu ya Rais Dkt Magufuli

0


Rais Dkt John Pombe Magufuli jana usiku alitengua uteuzi na kumrejesha nchini Balozi wa Tanzania nchini Canada, Alphayo Japani Kidata ambao uamuzi huo ulianza Novemba 5, 2018.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Faraji Kasidi Mnyepe, mbali na Rais kutengua uteuzi huo, pia alimvua Alphayo Kidata hadhi ya ubalozi.

Mbali na hatua zote hizo zilizochukuliwa, bado haijafahamika kuwa kiongozi huyo ambaye ndani ya miaka mitatu ya Rais Dkt Magufuli amseshika nyadhifa muhimu ni kitu gani amefanya kustahili adhabu hizo.

Tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani Novemba 5, 2015, Alphayo Kidata ameshika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

Nafasi hiyo aliiacha na kumpisha Dkt Yamungu Kayandabila, baada ya Kidata kuteuliwa na Rais Dkt Magufuli kuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Januari 2016.

Kidata hakukaa muda mrefu sana kwenye nafsi huyo ya kukaimu, kwani baadaye alithibitishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Machi 23, 2017, Rais Dkt Magufuli alimteua Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu, Ikulu akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Peter Ilomo ambaye alistaafu.

Tarehe 10 Januari 2018, Rais Dkt Magufuli alimteua Alphayo Kidata kuwa Balozi, lakini hakupangiwa kituo cha kazi wakati huo kutokana na taratibu kutokamilika, kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa.

Mei 10, 2018 Rais alimuapisha Alphayo Japani Kidata kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada. Balozi Kidata ambaye pia alikuwa akiiwakilisha Tanzania nchini Cuba alichukua nafasi iliyoachwa na Balozi Jack Mugendi Zoka ambaye alimaliza muda wake.

Meizi sitaa baada ya kuapishwa kwake na kuanza kazi, uteuzi wake (Kidata) umetengulia, amevuliwa hadhi ya ubalozi na kurejeshwa nchini kutoka Canada.

Kufuatia hatua hiyo, watu wengine wametoa maoni yao mitandaoni, huku jambo kubwa likiwa na kutofahamika kwa sababu hasa au kosa la balozi huyo.

Comments

Share.

About Author

Leave A Reply