Tuesday, March 19

Rais ateua Mwenyekiti wa Shirika la Nyumbu na Kamishna wa Fedha na Utawala wa Zimamoto

0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi Lut. Jen. Mstaafu Wyjones Mathew Kisamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumbu (Tanzania Automotive Technology Center).

Balozi Lut. Jen. Mstaafu Kisamba anachukua nafasi ya Prof. Burton Mwamila ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Mbaraka Sultan Semwanza kuwa Kamishna wa Utawala na Fedha katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

SACP Semwanza anachukua nafasi ya CF Michael Shija ambaye amestaafu.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 04 Desemba, 2018.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

04 Desemba, 2018

Comments

Share.

About Author

Leave A Reply