Saturday, August 17

Msanii wa Bongo Movie auza figo ili arekodi filamu

0


Msanii Erasto Kilowoko ‘Magumashi’ aliyetangaza kuuza figo yake moja kwa gharama ya shilingi milioni 25 ili apate fedha za kurekodi filamu yake.

Msanii wa maigizo na filamu Tanzania mwenyeji wa Mkoa wa Iringa, Erasto Kilowoko maarufu kama Magumashi Magumashi ameeleza kuwa anauza figo yake moja ili aweze kutimiza ndoto yake ya kurekodi filamu hapa nchini.

Msanii huyo ameeleza kuwa, lengo lake kubwa la kuuza figo ni kupata fedha itakayomwezesha kurekodi filamu yake mpya ambayo ina lengo la kuwaelimisha vijana kuhusu maisha katika jamii, uzalendo pamoja na uwajibikaji.

Magumashi ambae kwa sasa anajidhughulisha na kazi ya kinyozi mjini Iringa amesema kuwa anauza figo yake kwa garama ya shilingi million 25 na ameaidi kuwa kama atafanikiwa kuuza figo hiyo basi atatoa kiasi cha shilingi milioni 5 kwa serikali kama kodi ili kuongeza mapato kwa taifa.

“Nimekuwa nikiomba viongozi na makampuni mbalimbali wanisaidie kutimiza ndoto zangu lakini naona kimya. Nataka kuwa kioo cha jamii kwa kutoa elimu kupitia sanaa. Ninauza figo yangu moja kwa gharama ya shilingi milioni 25 na kama serikali inataka mapato nitawapa milioni 5. Shida yangu kubwa sio kujenga nyumba au kununua gari, ila kutimiza ndoto zangu,” alisema Magumashi.

Magumashi anasema kwamba ana uhakika kuwa soko la filamu Tanzania litakaa vizuri kwa sababu kiongozi wa nchi, Rais Dkt John Pombe Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuthibiti kazi za wasanii.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.