Friday, April 19

Matokeo ya Darasa la Saba yaliyotangazwa leo na NECTA

0


Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, huku kukiwa na ongezeko la ufaulu katika masomo ya Maarifa ya Jamii, Sayansi, Hisabati na Kiingereza

Wakati ufaulu katika masomo hayo ukiongezeka, ufaulu katika somo la Kiswahili umeshuka ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa NECTA, Charles Msonde amesema kuwa mikoa mitatu iliyoongoza kwa kufanya vizuri zaidi ni Dar es Salaam, Geita na Arusha.

Baraza hilo pia limefuta matokeo yote ya wanafunzi 357 waliobanika kuhusika na udanganyifu na kuzuia kutoa matokea ya watahiniwa 120 ambao walikuwa wakiumwa na watafanya mtihani mwaka 2019.

Kuona matokeo hayo, bonyeza hapa au hapa

Comments

Share.

About Author

Leave A Reply