Thursday, February 21

Marekani yakosoa hali ya kisiasa nchini Tanzania

0


Serikali ya Marekani imeeleza kusikitishwa na mmomonyoko wa haki za binadamu nchini Tanzania ambazo kwa kiasi kikubwa imeeleza zinachangiwa na sheria (ilizoziita kandamizi) ambazo zinaminya haki za kiraia, kutengeneza mazingira ya vitisho, na ubaguzi.

Taarifa hiyo ya Marekani imekuja ikiwa ni muendelezo wa Tanzania kukosolewa kutokana na kampeni ya kupinga ushoga iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambapo mataifa mengi ya magharibi yamechukulia hatua hiyo kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Aidha mbali na hao, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani jana Novemba 9 imeeleza kuwa kumekuwa na ukamataji na vitisho kwa raia wengine ambao wanatimiza haki yao ya kuzungumza, kujieleza pamoja na kukusanyika pamoja.

Aidha, kumomonyoka huko kwa haki za binadamu pamoja na kutofuatwa kwa utawala wa sheria, kuna pelekea nchi kutofikia malengo inayokusudia kwani kunakoseka amani,ulinzi pamoja na usalama, ilieleza taarifa hiyo.

Marekani imezisihi mamlaka nchini Tanzania kuchukua hatua stahiki kuhakikisha inalinda uhuru wa wananchi, asasi za kuraia, haki za binadamu na watetezi wa haki hizo, waandishi wa habari, wanaharakati wa kisiasa na watu wengine wote kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, kwani kwa pamoja wanamchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.

Aidha, taifa hilo limeitaka Tanzania kutekeleza matakwa ya sheria mbalimbali za kimataifa ambazo imesaini na kuridhia ili kulinda haki za raia na makundi mbalimbali ndani ya jamii.

Comments

Share.

About Author

Leave A Reply