Friday, July 19

Makundi 3 yanataka kumuangamiza RC Makonda- Mchungaji Mwingira

0


Dar es Salaam: Kiongozi wa Kanisa sa Efatha, Mchungaji Josephat Elias Mwingira amesema kuwa kuna makundi matatu ya watu wanataka kumuangamiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, lakini hawatafanikiwa.

“Kuna makundi matatu, nayaona uamepanga kukuangamiza kwa gharama kubwa, lakini leo nasimama kwa niaba yako mbele za Mungu aliye hai,” alisema mchungaji huyo.

Aidha baada ya kumfanyia maombi hayo, alimwambia kiongozi huyo kuwa atakuwa salama kwani Mungu atamlinda dhidi ya yeyote anayetaka kumdhuru.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametokwa na machozi wakati akizungumzia mmonyoko wa maadili nchini Tanzania, hasa katika jiji la Dar es Salaam, ambalo kwa siku za hivi karibuni limeshuhudia ongezeko kubwa la vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga).

Akizungumza katika ibada ya Jumapili katika Kanisa la Efatha linaloongozwa na Mchungaji Mwingira, RC Makonda amesema kuwa, watu wamekuwa hawasikii neno la Mungu na kwamba wamegeukia uzinzi na mambo mengine ambayo ni kinyume na misingi ya dini pamoja na maadili ya Mtanzania.

“Watu wanakataa neno la uzima, sheria ipo lakini watu hawaifuati. Watu wanaona raha kufanya uzinzi hawana muda wa kumtafuta Mungu,” alisema RC Makonda huku akitokwa na machozi.

RC Makonda amewataka waumini hao kuendelea kuiombea nchi ili kuweza kuepuka vitendo hivi, huku akiwataka wazazi kuwa karibu na watoto wao.

Comments

Share.

About Author

Leave A Reply