Tuesday, August 20

Maagizo aliyotoa Rais Dkt Magufuli kuhusu kuuawa kwa Mwanafunzi

0


Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia ya Akwilina Akwilini aliyeuawa baada ya kupigwa na risasi katika maandamano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Februari 16, 2017 eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam

Katika salamu hizo, Rais Dkt Magufuli amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho na hivyo ameviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT). Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu. Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili.”

Akwilina alikumbwa na umauti wakati Polisi walipokuwa wakitawanya maandamano ya CHADEMA walipotaka kwenda kwenye Ofisi za Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni kuhoji kwanini mawakala wao hawajaaapishwa.

Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa, wanawashikilia askari 6 ambao wametumia silaha za moto katika mchaguzi huu mdogo wa Kinondoni.

Aidha, Mambosasa amesema kwamba, CHADEMA waliwazuia Polisi kutekeleza wajibu wao ndio sababu nguvu ya ziada ilitumika kutawanya waandamanaji.

Amesema wanamtafuta Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe ili wamfikishe katika vyombo vya sheria.

Hadi sasa wafuasi wa CHADEMA 40 wamekamatwa na wanashikiliwa mpaka sasa kwa kuandamana katika uchaguzi wa marudio.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.