Tuesday, July 23

Jibu la Alikiba kuhusu kushiriki Wasafi Festival

0


Baada ya Diamond Platnumz kutangaza kuwa anatamani kushiriki pamoja na mwanamuziki Ali Kiba kwenye Tamasha la Muziki la Wasafi (Wasafi Festival) ambalo litaanza hivi karibuni, Alikiba amejibu na kusema anashukuru sana kwa mwaliko huo, lakini kwa sasa hata weza kutokana na kutingwa na mambo yake mengine.

Akizungumza wakati akitangaza tamasha hilo, Diamond Platnumz alisema kwamba litaanza Novemba 24 mwaka huu, ambapo litaanzania mkoani Mtwara. Ikiwa ni njia ya kuendelea kukuza vipaji na biashara, alisema angependa kushirikiana na wasanii wengine ambao miongoni mwao alimtaja Alikiba ambaye huonekana kama mshindani wake mkuu.

“Hili tamasha ni lakwetu sote kwa wasanii wote wa Kitanzania na katika tamasha hili ningefurahi sana kama kaka yangu Alikiba atakuwepo kwenye tamasha hili,” alisema Diamond

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba aliandika kuwa amepata salamu hizo na anashukuru sana, lakini atakuwa akizindua kinywaji chake cha Mofaya katika nchi nyingine.

“… ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrinkili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa

Aliongeza kuwa, uongozi unaomsimamia wa kampuni ya Rockstar Africa utaendelea kuwasiliana na WCB ili kutuweze kufanya hili jambo kubwa.

Comments

Share.

About Author

Leave A Reply