Friday, July 19

HIVIPUNDE: Mbunge wa Temeke atangaza kujiuzulu akiwa ndani ya Bunge

0


Mbunge wa Temeke kwa tiketi wa Chama cha Wananchi (CUF) Abdallah Mtolea ametangaza kujiuzulu ubunge na nafasi zake zote za uongozi ndani ya chama hicho kuanzia leo Novemba 15, 2018.

Akiyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma, Mtolea ameeleza kuwa, kwa muda mrefu sasa ndani ya chama hicho kumekuwa na mgogoro wa kiungozi ambao haufikii mwisho.

Baada ya kutangaza uamuzi huo, Mtolea alitoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Kujiuzulu huko kwa Mtolea kunakuja ikiwa leo ni siku ya mwisho iliyotangazwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa, ni mwisho wa kuwapokea wabunge na madiwani kutoka upinzani ambao watapewa nafasi za kugombea tena.

Uamuzi huo ulifikiwa katika Kikao cha Kamati Kuu Maalum jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti Rais John Magufuli.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, baada ya leo (Novemba 15) wabunge na madiwani watakaoomba kujiunga na CCM watapokelewa na kubaki kuwa wanachama wa kawaida.

“NEC imeelekeza kuwa tarehe 15 Novemba ndio itakuwa mwisho wa kupokea maombi ya uanachama wa CCM na kupewa dhamana ya uwakilishi kupitia tiketi ya CCM kwa wabunge na madiwani kutoka vyama vingine,” alisema Polepole na kuongeza:

Lakini tofauti na wabunge wengine wa upinzani waliojiuzulu, Abdallah Mtolea hakueleza kama atajiunga CCM ama la.

Comments

Share.

About Author

Leave A Reply