Saturday, August 17

Diamond aomboleza kuachwa na Zari

0


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye ameupaisha muziki wa Tanzania Afrika na maeneo mengine duniani kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata, Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platinumz’ ameweka wazi hisia zake baada ya kuachwa na aliyekuwa mpenzi wake Zarinah Hassan maarufu ‘Zari the Boss Lady’.

Diamond ameonyesha wazi kuumizwa na kitendo cha mahusiano baina yake na mzazi mwenzake kuvunjika, ambapo katika ukurasa wake wa instagram ameweka mfululizo wa ‘post’ akilalamikia kitendo hicho.

Katika post moja ambayo ameiambatanisha na video ya wimbo wa Nimekuzoea ameandika “Hayo Mashairi Chaganya na Ua Jeusi…… Dah @mbosso_naona Kama Ulintabiria Mdogo angu😭😥🤦‍♂️”

 

Katika post iliyofuatia Diamond aliweka video ya wimbo wa Mapacha Watatu wenye jina Kuachwa na kuandika “Dah, Kuna nyimbo zingine ziliandikwaga jamani…Wadau Dua zenu Muhimu…. Maana naona kabisa mwezi wa Tatu Siuoni😭

 

Muda mfupi uliopita ameongeza post nyingine ambayo ameweka kipande cha wimbo wake wa ‘Sikomi’ na kuandika “Unajua Nyimbo zingine Unaziimba ila Hata we mwenyewe zinakuingia Baadae😟…. Anyways 28 Days Before the Feveal of #AboyFromTandaleAlbum!🔥 #SikoMi Bonus Track on #AboyFromTandale

 

Jumatano, Februari 14, mwaka huu siku ya wapendanao ‘Valentines’ Day’, siku ambayo wapenzi wengi katika maeneo mbali mbali ulimwenguni kote huitumia konyeshana hisia zao na kufanyiana mambo mazuri yatakayoboresha mapenzi yao, kwa upande wa mrembo Zari ilikuwa tofauti, kwani aliitumia siku hiyo kueleza uamuzi wake wa kuachaana na Diamond, kwa kile alichokitaja kuwa ameshindwa kuvumilia vitendo vya msanii huyo kukutwa na kashfa nyingi za kutoka na wanawake wengine.

Hata hivyo, Diamond bado hajaweka wazi mpango wake wa kimaisha baada ya kuvunjika kwa mahusiano baina ya wawili hao waliopendana na kufikia hatua ya kuzaa watoto wawili Tiffah na Nylan.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.