Saturday, August 17

BREAKING: Sugu ahukumiwa kifungo jela

0


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, imewahukumu kifungo cha miezi mitano jela Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais Dkt John pombe Magufuli.

Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26, 2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite.

Sugu na Masonga wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge, jijini Mbeya.

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.