Saturday, August 17

IFISI HOSPITAL FC YAKANYAGA NYAYO ZA TUKUYU STAR, YATUA MJINI RUNGWE KUWAKABILI

0


 Katibu wa Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Mbalizi Ifisi, Emmanuel Martin.NA MWANDISHI WETU, RUNGWE 

IKIWA imebakia siku moja kushuhudiwa kwa mtanange wa mzunguko wa mwisho wa Daraja la Tatu Sita bora, kati ya timu ya Tukuyu Star na Ifisi Hospital FC, timu ya Ifisi yenye makao yake makuu Mbalizi Mbeya Vijijini imetua mjini Tukuyu leo. 

Wakizungumza na waandishi wa habari leo,  baadhi ya viongozi wa Ifisi FC ambao wapo eneo la Ushirika nje kidogo ya mji wa Tukuyu, wamesema wapo imara na hawana majeruhi hata mmoja. 

Timu hiyo ambayo imeongozana na vigogo wa Hospitali ya wilaya ya Mbeya na baadhi ya maafisa wa idara mbalimbali kutoka ngazi ya Mkoa. 

Katibu wa Hospitali ya Mbalizi Ifisi ambao ni wamiliki wa timu hiyo Emmanuel Martin amesema wanaijua vema Tukuyu Star hivyo wana imani kuwa wataibuka washindi. 

“Ninayasema haya hapa Tukuyu kwasababu tuna uhakika kwa rekodi ambayo tunayo. Wababe wote wa Tukuyu sisi tuliwachapa wakiwemo Syukula na uzuri marefa hawaibebi timu yeyote wanachezasha katika usawa” alisema Katibu huyo. 

Afisa Habari wa timu hiyo Gordon Kalulunga Maarufu kwa jina la mzee wa Nyikani, amesema lengo la timu yao kuwahi Mjini Tukuyu ni kutaka wachezaji wazoee hali ya hewa ya Tukuyu ambayo ni baridi tofauti na maskani yao Mjini Mbalizi.

Baada ya kufika leo mjini Tukuyu, timu hiyo imeahidi kukutana tena na waandishi wa habari kesho katika hoteli ya Land Mark ili uueleza umma kuhusu uwanja watakao utumia kufanya mazoezi na kuwaomba wapenzi wa soka kujitokeza kuangalia kandanda ya timu hizo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.