Monday, August 26

WAZIRI JAFO ATOA AGIZO KILOLO KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA

0


Waziri Ofisi ya Rais , tawala za mikoa na serikali za mitaa, TAMISEMI, Mh. Selemani Jaffo amefurahishwa na ujenzi wenye ubora wa hospitali ya kisasa ya wilaya ya kilolo na kuagiza wakandarasi wanaojenga hospitali za wilaya ya Kilolo na ile ya Iringa kukamilisha ujenzi huo kabla ya mwezi wa saba, Mwandishi Francis Godwin anaripoti kutoka Iringa .

Waziri Jaffo, ametoa
maagizo hayo akiwa katika ziara ya siku moja mkoani Iringa, wakati ametembelea ujenzi
wa hospitali ya wilaya ya Kilolo pamoja na halmashauri ya Iringa vijijini
kwenye kijiji cha Igodi Kafu  Kata ya Pawaga.

Amesema serikali
inajenga zaidi ya hospitali 67 za wilaya nchini ili kuhakikisha wananchi
wanapunguziwa changamoto ya huduma za afya kwenye maeneo yasiyofikika kirahisi  ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma ya mama na
motto.

Aidha Mh. Jaffo
amewaagiza wale wote ambao wamehusika na wizi wa sementi kwenye ujenzi wa
hospitali wilaya halmashauri ya Iringa, Igodi kafu wachukuliwe hatua za
kisheria, kwakuwa wanachelewesha ujenzi wa hospitali hiyo ambayo inajengwa  umbali wa km 75 kutoka Manispaa ya Iringa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ali Hapi akitoa pongezi kwa serikali amesema, uongozi wa mkoa pamoja na wilaya hizo mbili wamekubaliana na wakandarasi kuhakikisha ujenzi huo unaisha kabla ya Juni 15 mwaka huu, ili kuharakatisha utoaji wa huduma ya Afya mkoani humo.

Hata hivyo, akizungumza kwa niaba  ya wananchi mkazi wa Kijiji cha Igodi Kafu Manyota Issa Magina amesema wamekuwa wakitembea zaidi ya kilomita 75 mpaka Iringa Mjini, ili kupata huduma za afya na kwamba ujenzi huo ni Ukombozi katika maisha yao.


Share.

About Author

Leave A Reply