Saturday, August 24

WANAFUNZI WAWILI SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA KULIWAKILISHA TAIFA KWENYE KONGAMANO LA DUNIA

0


Wanafunzi  wawili   wa  shule  ya msingi   Southern Highlands  Mafinga   mkoani Iringa  kuziwakilisha  shule  zote za Tanzania  nchini Finland katika kongamano la mazingira  kwa  shule  za msingi Duniani 

Akizungumza jana  juu ya ziara 
hiyo kiongozi  wa  wanafunzi hao nchini Finland ,mkurugenzi
wa  shule 
hiyo  ya  Southern Highnalnds  Mafinga 
Kitova Mungai
 
alisema kuwa    shule  hiyo ni miongoni mwa   shule wanachama wa  Klabu 
za mazingira  duniani na  kuteuliwa kwa 
wanafunzi hao   kumetokana na
ziara ya   waratibu wa  kongamano 
hilo ambao walifika  kupema
uwezo  wa klabu zote  nchini .

Hivyo 
baada ya  kuvutiwa na jitihada
zinazofanywa na klabu ya shule    yake katika 
utoaji wa elimu ya  mazingira  na 
ufundishaji wa masomo ya 
ujasiliamali  kwa wanafunzi  ndipo 
wameweza  kutuma mwaliko  kwa wanafunzi 
wawili na kiongozi  mmoja
ambao  watakwenda  kushiriki kongamano hilo  kwa muda wa siku 10  safari ambayo itaanza jumanne wiki hii.

‘’ Tunategemea  kukutana na 
wawakilishi  kutoka  nchi mbali mbali  duniani kama china ,Japan, Brazil ,Marekani
,China ,Uganda , Kenya  na nchi
nyingine  nyingi ila  tunaimani kubwa ya  kuwakilisha 
vema Tanzania kwani   watoto ambao
wamechaguliwa  kwenda  katika kongamano  hilo 
wanauwezo mkubwa sana katika 
elimu ya mazingira “  alisema
Mungai

Alisema 
watoto hao  na  wenzao wamekuwa mbele  kuhifadhi mazingira ya Shule  ikiwa ni pamoja na uoteshaji wa miche ya miti
 na 
kuipata shuleni hapo na majumbani kwao  na  kwao
 suala la 
uhifadhi  wa mazingira  ni shughuli yao ambao  hata wakipewa nafasi ya kufundisha  wenzao wamekuwa wakifanya  vizuri.

Mungai alisema  kuwa 
Tnzania ni imekuwa mbele katika 
vita  dhidi ya mabadiliko ya Tabia
nchi na  kuwa hata  mkakati wa serikali wa  kuzuia mifuko ya  rambo ni mkakati ambao  wanafunzi 
hao   wamekuwa  wakifundishwa 
namna ya  kutunza mazingira  pasipo 
kutumia mifuko hatarishi ya mazingira 
na kuwa kupitia kongamano hilo 
watapata kuwasilisha mbinu mbali mbali za  utunzaji wa mazingira .

Akizungumza wakati
akiwakabidhi bendera ya Taifa  wanafunzi
hao na kiongozi wao  kwa  niba ya 
serikali ya  wilaya ya wilaya ya  Mufindi 
mwenyekiti wa  Halmashauri ya
Mufindi Festo Mgina alisema kuwa  heshima 
ambayo  shule  hiyo 
ya  Southern Highnalnds  Mafinga 
imepata  ni kubwa kwa  wilaya 
,mkoa na Taifa kwa  ujumla .

“  Huu 
ni  mwaliko  wa heshima 
kubwa kwa wilaya  yetu na
mkoa  lakini kwa Taifa  letu  kualikwa
katika kongamano kubwa kama  hili  la  kujadili masuala ya mazingira  duniani 
heshima    hii sisi kama   viongozi 
tunajivunia na tunapongeza 
shule  kwa   kuteuliwa kuwakilisha Taifa “  alisema 
Mgina

Kuwa  mwaliko 
huo umekuja  wakati Taifa  liko katika 
harakati ya kuhakikisha  mazingira  yanatunzwa na 
kukabiliana na changamoto zinazoweza 
kujitokeza kutokana na  mabadiliko
ya tabia nchi  hata  kuanza mchakato  wa  
kuondoa sokoni mifuko ya rambo ambayo ni moja ya  vikwazo 
vya mazingira .

HIvyo  aliagiza 
wakuu wa  shule za msingi
katika  wilaya ya  Mufindi 
kuhakikisha  wanafika katika shule
ya Southern Highnalnds  Mafinga   ili 
kujifunza  yale  ambayo 
wanafunzi  hao wawili watarudi
nayo kutoka katika mkutano  huo  mkubwa nchini Finland.

“tunataka elimu  na aagizo 
ambayo yatatolewa katika  mkutano
huo wa dunia nchini Finland  vijana
hao  wakirudi  basi 
kuweza  kusambaza kwa wenzao
kwenye shule zetu  zote za MUfindi ikiwa
ni pamoja na wakuu wa shule  kufika
kujifunza  ili  kila shule kuweza  kujifunza 
elimu  hiyo kwa faida ya  mazingira ya maeneo yao “  alisema Mgina .

Kwa 
upande wao wanafunzi watakaowakilisha Taifa katika kongamano hilo Maria Wambura  na  Stevin Sanga 
ambao ni wanafunzi wa  darasa la
saba katika  shule hiyo walisema   kuwa 
kuteuliwa kwao  katika  kongamano hilo si nafasi ya bahati mbaya
kwani wanauhakika  wa  kuliwakilisha 
vizuri Taifa  katika  kongamano hilo na kile ambacho
watakipata  watakuja  kutumia 
kutoa elimu kwa wanafunzi wenzao nchini .

Share.

About Author

Leave A Reply