Sunday, August 25

ASKOFU BLASTON GAVILE AONYA WANAOLALAMIKA VYUMA KUKAZA ,BALOZI DKT CHANA ATOA NENO …

0


Askofu wa  kanisa la  kiinjili la  kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya  Iringa Blaston Gavile atuma  salama tano  nzito za Pasaka ikiwemo ya  tahadhali  kwa  waumini wa kanisa hilo na wananchi kutumia vizuri  chakula watakachovuna na kile  walicoweka akiba kwani   kutokana na  hali ya mvua kunyesha kwa  kusuasua  pia  kuwataka  waumini kuacha kuinga kulalamika kuwa  vyuma vimekaza anaripoti mwandishi wetu FRancis Godwin kutoka mkoani Iringa

Askofu  Gavile  alitoa  salama   hizo leo kupitia  waumini wa kanisa  hilo usharika wa kanisa kuu   wakati  akitoa salam  za pasaka mara baada ya  kumalizika kwa ibada ya Pasaka ibada iliyohudhuriwa na balozi wa  Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Chana .

Alisema kuwa  hali ya  mvua kwa mwaka huu  2019  haijawa  ya  kuridhisha   katika maeneo mengi   na  kuna baadhi ya maeneo yamepata neema ya  chakula  na  sehemu  nyingine  mazao yamekauka  yakiwa katika hatua ya awali kabisa ya ukuaji  wake  hivyo  hawatavuna kabisa .

” Sisi  tuliyebahatika   ambao  tunadalili ya kuvuna  tutunze chakula hicho ili  kitufae wakati wa njaa na kuwasaidia  wengine ambao hawajabahatika kuvunja  kutokana na ukame “

Katika   salam yake ya  pili  alisema kuwa  katika jamii  yetu ya watanzania  kumeibuka na hali ya  kulalamika  na  kunung’unika  kwamba  hali ya  uchumi ni ngumu ” Nyuma vimekaza”  hivyo  aliwaomba  waumini wa kanisa hilo  kuepuka kuingia wala kuchangia katika hali   hiyo ya kulalamika  bali  kufanya kazi kwa bidii na  maarifa  kutumia fursa  zilizopo  katika  kuinua hali ya  kipato chao na familia  kwa ujumla .

Aidha  alisema  taarifa zinaonyesha  kwamba mkoa wa Iringa  ni miongoni mwa  mikoa  inayotajwa  kwa sifa  mbaya  hasa ya  inayohusiana na vitendo vya ukatili  kwa watoto ,alawiti na mauwaji ya  watoto  wadogo  ambayo  lengo lake ni  kujipatia mali  kwa njia ya  ushirikiana   kuwa wao kama kanisa  wanakemea  vitendo hivyo kwa  nguvu  zote na sala zote .

” Tuendelee  kuiombea dayosisi yetu ya  Iringa  kwa mapana yote  ili  iendelee  kutekeleza vizuri  mpango mkakati  wa wake  wa miaka 10  2018-2028 na  kuombea vitendo  vyote vya kikatili zisijitokeze katika  mkoa  wetu  tuendelee kuomba  na  kuombea nchi yetu Tanzania  kwa mapana yote  ” alisema askofu Gavile

Kuwa    Taifa linaelekea katika  uchaguzi wa serikali za mitaa  uchaguzi utakaofanyika  mwezi  Octoba mwaka 2019  na uchaguzi mkuu  utakaofanyika mwaka 2020  hivyo kazi ya kanisa  ni  kuendelea kuombea chaguzi  hizo  zote na  kuwa  japo uchaguzi mkuu ni mwakani ila maandalizi ya uchaguzi huo  huanza sasa na  njia pekee ya kupata  viongozi  wenye hofu ya Mungu  watakaoongoza  jamii ya  kitanzania ni kufanya maombi .

” Tuendelee  kuomba na   kumwombea Rais wa  jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt John Magufuli  kwa kazi  nzuri  kubwa anayoendelea kuifanya  ,tukiomba pia kwa ajili ya wasaidizi wake  zaidi  sana tutaendelea  kuomba kwa ajili ya amani na utulivu wa  nchi  yetu Tanzania “
Awali  akitoa  salam za watanzania  waishio nchini  Kenya na  serikali ya Kenya  balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Chana  alisema kuwa  uongozi wa  serikali ya Kenya akiwemo  Rais wa nchini  hiyo  wanawasalimia sana Watanzania na  wanapongeza amani na jitihada za  watanzania katika kufanya kazi.

Hata  hivyo  aliwaomba  watanzana  kuendelea  kuongeza  nguvu katika  uzalishaji wa  mazao mbali mbali yakiwemo ya  mazao ya chakula kwani  alisema  hali ya mvua  Kenya  si nzuri na kuna dalili  kubwa ya  kuwa na upungufu mkubwa wa mazao ya chakula  kutokana na mvua  kutonyesha  vizuri mwaka  huu na  hivyo  watahitaji  chakula  kutoka Tanzania .

” Kenya  mvua mwaka huu haijanyesha   hivyo chakula  wananchi  wake  watahitaji zaidi kutoka Tanzania nawaombeni  endelee  kulima kwa   juhudi na msiwe na hofu  juu ya soko kwani Tanzania na Kenya  ni  jirani hivyo  watategemea chakula  kutoka Tanzania”

Aidha  Balozi  Dkt  Chana  alisema  kazi kubwa  inayoendelea  kufanywa na Rais Dkt Magufuli   imekuwa ikililetea  heshima  kubwa Taifa la Tanzania ndani ya Tanzania na hata  nchini  Kenya kwani  watanzania  waliopo Kenya  wanafarijika sana na  heshima  kubwa ambayo Rais  ameweza  kuliletea Taifa la Tanzania.

Share.

About Author

Leave A Reply