Tuesday, August 20

UNASUMBUKA NA HANGOVER? TUMIA NJIA HII KUIMALIZA. TIBA!!!

0


Inawezekana wewe ni kati ya watu wanaopenda kupiga vyombo (Pombe) kwa kiasi kikubwa, inawezekana ni starehe yako lakini unakerwa sana na hali unayoamka nayo asubuhi, hangover, wengine kwa kiswahili kisicho rasmi sana wanaita mnng’inio na umekuwa ukipata taabu sana kuimaliza hiyo hali pengine kwa kunywa mchemsho au kutoa lock angalau kwa kunywa tena pombe kidogo.

Pamoja na njia zote uzitumiazo kumaliza hiyo hali ya mning’inio, Fichuo leo inakupatia tiba halisi, rahisi na ya asili ya kukuondolea hangover.
Kuna mchanganyiko wa kinywaji-lishe unaitwa BANANA MILKSHAKE, hiki ni kinywaji-lishe kinachotengenezwa kwa mchanganyiko wa maziwa fresh, ndizi mbivu pamoja na asali. Ukipata kinywaji-lishe hiki angalau kikombe/glasi moja katika asubuhi uliyoamka na hangover itaamsha nguvu zako na kutoa uchovu unaokupatia usumbufu.
Kwanini hii ni tiba? Kwakuwa ndizi mbivu husaidia kutuliza tumbo na kumaliza kilevi lichosalia mwilini wakati asali kazi yake ni kusawazisha na kujenga viwango vya sukari iliyoharibika mwilini.
Maziwa yenyewe tunafahamu kwamba yana vitamins zenye msaada mkubwa katika mwili wa binadamu, ambazo ni A, D, E na K

BANANA MILKSHAKE inatengenezwaje? Jifunze hapa;

Katika kutengeneza BANANA MILKSHAKE utahitaji kuwa na maziwa mabichi angalau lita moja, ndizi mbivu kubwa 2 au ndizi kisukari 4 (ndizi mbivu ndogondogo) na asali angalau vijiko vitatu vya chai. (japo hapa pia inategemeana na kiasi cha uzito na ladha uitakayo katika kinywaji-lishe chako.
Chemsha maziwa vizuri kisha wacha yapoe kabisa, kisha yatie katika brenda na uchanganye na ndizi pamoja na asali na ukoroge pamoja. baada ya hapo unaweza kutia katika friji ili upate kiwango cha ubaridi utakaoutaka haraka. Baada ya hapo inakuwa tayari kwa matumizi. Ikikusaidia saidi na wengine kama Fichuo ilivyokusaidia.

Burudika kidogo na wimbo Hangover toka kwa PSY na SNOOPRead More

Share.

About Author

Comments are closed.