Monday, June 17

Utaalamu katika IT: Application Programmer

0Application Programmer huhusika na kudesign, kutest programu katika upande wa logic, pia huandaa documentation na kutengeneza programu kwa ajili ya matumizi ya kampuni husika.

Kazi Afanyazo

 • Anafanya coding, testing, debugging, documenting na installation ya programu.

 • Anatumia lugha maalumu za computer ili kuongeza ufanisi wa programu zinazoendelea kufanya kazi.

 • Anafuatilia ufanyaji kazi wa ufanisi wa programu zote zinazofanya kazi, na kushughulikia mapungufu yote yanayojitokeza.

 • Anatumia mahitaji maalumu ambayo amepewa na kampuni, na kutengeneza programu mbazo zitasaidia kutimiza malengo hayo…mfano: Vodacom wanapotaka kuongeza offer kwenye menu ya MPESA watahitaji kumuona huyu mtu.

 • Muda wote huutumia kujiupdate ili kuhakikisha ya kwamba mifumo yote ya kampuni inafanya kazi katika viwango vya kisasa.

 • Hujifunza na kuchambua kazi mbali mbali za kampuni na kutoa mchango wake katika kuboresha mifumo husika ili kuleta ufanisi wa hali ya juu katika MIS(Management Information Systems).
Vigezo Vya Kazi.
 • Awe na uelewa mzuri wa software na hardware( Technical Capacity)

 • Awe na uwezo mzuri wa kutatua changamoto zote zinazojitokeza kwa kutengeneza majawabu ya kiteknolojia.(Problem Solving/ Analysis)

 • Awe na uwezo wa kujisamamia mwenyewe na kuchukua hatua mbali mbali za kiutendaji(Initiative).

 • Uwe na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wengine na kuweza kuwasilisha kile ambacho unataka kufanya kwa lugha nyepesi na ya kueleweka zaidi.

 • Uwe vizuri katika kutumia muda vizuri.


Elimu na Mafunzo
Uwe amepitia kozi zifuatazo , lakini pia awe na ujuzi binafsi wa lugha za computer kama zifuatazo Java, Android, PHP, SQL, HTML,CSS, ASP.Net, Javascript, Python, VB.Net etc.

Bachelor in Computer Science

Bachelor in Information Systems

Bachelor in Software Engineering

Bachelor in Computer Engineering

Bachelor in Information Technology

Na kozi nyingine zinazofanana na hizo hapo juu. 
Kwa maelezo, msaada au ushauri zaidi usisite kuzungumza nami. 
elisanteshibanda@yahoo.comRead More

Share.

About Author

Leave A Reply