Sunday, August 25

Pata Ushauri Wa Kiteknolojia

0


Ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kufanya mabadiliko yeyote yale yanahusiana na teknolojia…

Ni kwa sababu zifuatazo
Usalama
Katika ulimwengu wa leo, kuna wizi mwingi sana katika mitandao haswa katika teknolojia inayohusiana na kompyuta, na hata tuna taarifa ya kwamza hapa Tanzania tupo katika nchi chache duniani ambapo wizi mwingi hutokea.

Mabadiliko ya Teknolojia
Teknolojia hubadilika mara kwa mara, unayotaka kutumia au kununua leo inaweza ikawa ishatoka katika usasa na ni ya zamani na inatakiwa kubadilishwa kutokana na sababu za kiusalama. Kwa hiyo ukajikuta umepoteza pesa zako nyingi.

Sheria na Matakwa ya Nchi Husika
Sio kila teknolojia unaweza kuitumia Tanzania au nchi nyingine na hata kuna njia ya kutengeneza system yeyote ili ikidhi viwango vya nchi husika mfano katika maswala ya usajili wa tovuti kwa Tanzania kuna sheria mahususi ambazo ni za kipekee kabisa hazipo duniani kote.

Kupata Wataalamu Husika
Sio kila aliye kwenye fani hii ni bora na anafaa kutumiwa, wengine wana uwezo tofauti na utawapata kulingana na mfuko wako.

Read More

Share.

About Author

Leave A Reply