Thursday, August 22

USHAURI WAKITAALAMU ULIJADILIWA KWENYE KONGAMANO LA ELIMU, ARUSHA.

0


Mkurugenzi wa Freemind Co.Ltd akielimisha kuhusu Ushauri Wakitaalamu na umuhimu wake katika elimu na maendeleo ya mtu binafsi.Kimsingi alisema yeye na wenzake kwenye kampuni yao wanasaidia wateja wao kutambua thamani yao, kubaini uwezo walionao na kushauriana njia njema ya kufikia malengo kwa mtu husika. Alishangazwa sana na wanadamu kujaliwa akili ila wanaitumia akili hiyo kujiwekea vikwanzo na mipaka katika mambo na majukumu yao, alisema “ninashangaa sana wanadamu wengi hutumia muda mwingi kutafuta vikwazo na kuwekeana mipaka, wakati miti yenyewe inakuwa bila mipaka, wanyama wanaishi vema”. Alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau wa elimu hasa wanafunzi kutumia taasisi yao kupata ushauri wakitaalamu.  

Mkurugenzi wa Freemind Co.Ltd akisisitiza jambo kuhusu ushauri wa kitaalamu.

Majadiliano kati ya mdau wetu Godfrey Tawete na Godrich Izack.

Wadau wakiwa kwenye majadiliano ya kikundi kuhusu mada za elimu yetu.


Read More

Share.

About Author

Comments are closed.