Sunday, August 25

MWANAFUNZI ANTHONY PETRO APATA MTETEZI

0


Mfadhili wa kumsomesha Anthony Petro (10) amepatikana. Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Aidan Bahama amesema mtoto  amepata mfadhili huyo Isihaka Msuya aliyejitolea kumwendeleza mtoto Anthony hadi Mwenyezi Mungu atakapomfikisha pale anapohitaji kufika na atampatia mahitaji muhimu ya haki za binadamu.

Mtoto huyo Anthony Petro ambaye pia ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ngundusi, hivi karibuni alijulikana kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari baada ya kumzuia baba yake mzazi aliyetaka kuuza shamba.

Aidha inaelezwa kuwa maisha ya familia ya mtoto huyo ni ya shida kiasi cha kukosa mlo wa mchana kwani baba yao hana uwezo wa kifedha na wakati mwingine familia hiyo hutumia maparachichi kama mlo wa mchana au usikuRead More

Share.

About Author

Comments are closed.