Friday, August 23

Zifahamu ‘Passwords’ zinazodukuliwa zaidi mtandaoni

0


Tumia neno la siri lisilotambulika kirahisi ili kuzidi kujilinda dhidi ya uhalifu wa mtandaoni. Picha|Mtandao.

  • Ni zile zinazotumia namba na mwaka wa kuzaliwa bila kuchanganya na herufi au alama.
  • Wadau wa teknolojia washauri watumiaji wa intaneti kuchukua tahadhari ya usalama kwa kutengeneza ‘passward’ zisizotambulika kirahisi. 

Dar es Salaam. Licha uhalifu wa mtandao kuongezeka duniani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utumiaji wa neno la siri (Password) dhaifu katika akaunti za mitandaoni lakini bado watu wanaendelea kutumia ‘passward’ hizo, jambo linalowaweka zaidi katika hatari ya kupata majanga.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Kituo cha Taifa cha Uingereza cha Usalama Mtandaoni (NCSC) imeweka wazi passwards ambazo zimekuwa zikivujishwa zaidi na wadukuaji mtandaoni kutokana na urahisi wa kuzitambua. 
Ripoti hiyo imetumia sampuli ya passward 100,000 kutoka kanzidata ya Have I Been Pwned ambayo inatumika kutambua passwords zipi zinazodukuliwa zaidi duniani.  

Katika uchambuzi wa matokeo ya utafiti huo, imebainika kuwa password zinazodukuliwa zaidi ni zile zenye nAmba kuanzia 1 hadi 10 na herufi kama ‘passward’. 

Katika matokeo yake umeorodhesha passwords tano ambazo zilivujishwa zaidi katika matumizi ya data (data breaches) ambapo ni pamoja na 123456  ambayo imekutwa na watumiaji 23.2 milioni, 123456789 (7.7 milioni). 

Aina nyingine ni neno qwerty (3.8 milioni), Password linatumiwa na watu 3.6 milioni na 111111 (3.1 milioni).


Ripoti hiyo pia imeweka wazi aina 10 za passwords zinazongoza kwa kudukuliwa zaidi na wahalifu ili kupata taarifa za watumiaji wa intaneti duniani katika akaunti zao za mitandao ya kijamii na huduma nyingine za mtandaoni kama barua pepe.

Passwords hizo ni 12345678, abc123, 1234567, password1, na 12345. Passwards nyingine ni zile zinazotumia majina ya ashley, michael, blink182, 50cent, superman, naruto na tigger.

Kutokana na watu wengi kuendelea kupuuzia kuwa na neno la siri lisilotambulika kirahisi wanazidi kujiweka katika hatari ya kushambuliwa na wahalifu mtandaoni na usalama wao kuwa shakani. 

Mkurugenzi wa teknolojia wa NCSC, Ian Levy katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jumapili (Aprili 21, 2019) wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo amesema watu wanatakiwa kuchukua hatua kujilinda mtandaoni kwa kuweka neno la siri ambalo litakuwa kama ukuta  ambao hauwezi kuingilika kirahisi na wahalifu. 

“Kutumia nywila za ambazo ni ngumu kwa mtu kufikiri ni hatua ya kwanza. tunapendekeza mtu kuchanganya maneno matatu  tofauti. Tumia maneno kwa ubunifu ambayo utayakumbuka na ambayo watu hawataweza kufirikiria kiurahisi,” amesema Levy.

Info.masshele@gmail.com

Share.

About Author

Leave A Reply