Friday, August 23

WIZI WA MAFUTA YA TRANSFOMA TUTAWACHUKUKLIWA KAMA WAHALIFU WAANOTUMIA SILAHA: KMANDA MAMBOSASA

0


 KAMANDA
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akiwa na Meneja
wa
Usalama na Upelelezi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw.
Maxmillian Birigi, akiwaonyesha waandishi wa habari shehena ya madumu
yenye mafuta ya transfoma.

 Meneja wa
Usalama na Upelelezi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw. Maxmillian Birigi, akizunhumza

 KAMANDA
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akizunhumza na waandishi wa habari

 KAMANDA
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akiwaonyesha
waandishi wa habari baadhi ya miundombinu ya TANESCO iliyoharibiwa na
wahalifu hao. ikiwa ni pamoja na mashine za kuchomelea za wahalifu hao.

 KAMANDA
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akiwa na Meneja
wa
Usalama na Upelelezi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw.
Maxmillian Birigi, akiwaonyesha waandishi wa habari shehena ya madumu
yenye mafuta ya transfoma.

NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said

KAMANDA
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameonya kuwa kuanzia
sasa mtu yeyote anayehujumu miundombinu ya TANESCO hatabaki salama na polisi
itamchukulia kama  muhalifu anayetumia
silaha.

Kamanda
Mambosasa ameyasema hayo leo Aprili 30, 2019 kwenye Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi
(Central) jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wake wa pamoja na Meneja wa
Usalama na Upelelezi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw. Maxmillian Birigi,
baada ya maafisa usalama wa shirika hilo kwa kushirikiana na polisi kunasa
mtandao wa wahalifu walioiba kiasi kikubwa cha mafuta ya transfoma ikiwa ni
pamoja na vyuma vinavyojenga transfoma jijini Dar es Salaam.

“Madhara
wanayosababisha ni zaidi ya uhalifu wa kutumia silaha, kwa sababu wanaharibu
uchumi wa nchi, na wanafikia mahali wanaharibu vyombo mbalimbali vinavyotumiwa
na wananchi.” Alisema Kamanda Mambosasa.

Kamanda
Mambosasa alisema Aprili 25, 2019 majira ya saa 5 usiku  jeshi la polisi kwa kushirikiana na maafisa wa
usalama wa TANESCO waliendesha operesheni ya kuwasaka watu wanaohujumu
miundombinu ya Shirika hilo katika maeneo mbalimbali ya jiji na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa 9.

“Mtuhumiwa
mmoja akiwa katika ghala la TANESCO lililoko eneo la Kigamboni alikutwa akiiba
mafuta kwenye transfoma namba T26840 aina ya TCO ya mwaka 2007.” Alisema.

Mtuhumiwa
baada ya kuhojiwa kwa kina, alitaja watuhumiwa wengine nane anaoendesha uhalifu
huo na baada ya polisi kuwatia mbaroni walisema mafuta hayo humuuzia mtu mmoja
ambaye walisema huyachanganya mafuta hayo na vimiminika vingine kisha kutengeneza
mafuta ya oil ambayo huyapa majina ya makampuni mbalimbali ya mafuta yanayouza
vilainishi vya mitambo na magari.

“Baada
ya kufika kwenye ghala na maduka yaliyo eneo la Tabata Dampo, polisi kwa
kushirikiana na maafisa hao wa TANESCO walikamata shehena ya madumu 68 ya lita
20 za makampuni mbalimbali ya mafuta, hata hivyo mshukiwa mkuu anayenunua
mafuta hayo alifanikiwa kutoroka na msako wa kumtia mbaroni unaendelea.”
Alisema.

Katika
upekuzi huo polisi pia walifanikiwa kukamata mapipa mawili yenye ujazo wa lita
200 yakiwa na mafuta ya transfoma.

Katika
muednelezo wa operesheni hiyo, Kamanda Mambosasa alisema pia polisi ilifanikiwa
kuwakamata watuhumiwa wawili wakiwa na vibati maalum vinavyokaa ndani ya
transfoma vinavyosaidia kuzalisha umeme na pia zilikamatwa mashine tano za
kuchomelea zilizotengenezwa kienyeji ambazo ni matokeo ya wizi wa vibati hivyo
vya transfoma.

“Katika
mahojiano walisema vibati hivyo huvitumia kutengenezea mashine za kuchomelea
yaani welding machines, wanaeda kuharibu
miundombinu ya TANESCO wapate hivyo vipati kwa ajili ya kutengeneza mashine
hizo hili hatutakubali.” Aliaapa Kamanda Mambosasa.

KWA
upande wake, Meneja wa Usalama na Upelelezi wa TANESCO Bw. Maxmillian Birigi,
yeye alisema ili kupata mafuta ya transfoma, lazima uivunje kwanza transfoma
yenyewe ili uweze kuyapata mafuta yaliyoko mle ndani.

Transfoma
ikiisha mafuta mafuta na kwasababu moto unazidi kuingia lazima ile transfoma
ilipuke na kuwaka moto.

“Athari
zake kubwa mbili ni pamoja na TANESCO kununua transfoma nyingine ili kurudisha
huduma ya umeme kwa wananchi lakini wakati Shirika likifanya jitihada za
kurudhisha huduma hiyo, wananchi watakosa huduma ya umeme kwa hivyo mtaweza
kuona kwa ksiai gani hawa watu ni wahujumu uchumi kwelikweli kama alivyosema
Kamanda Mambosasa.” Alisema Bw. Birigi.

 

Share.

About Author

Leave A Reply