Thursday, February 21

WAZIRI MKUU AWAONYA WAAGIZAJI WA TAULO ZA KIKE

0


 


*Ni wale wazaoziuza kwa bei ya juu licha ya Serikali kuziondolea kodi


*Asisitiza kwamba Serikali haitasita kuwafutia leseni zao za uagizaji
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amewatakabaadhi ya waagizaji wa taulo za kike
ambao wanaziuza kwa bei ya juu licha ya kufutwa kwa kodi, waache mara
moja na Serikali haitasita kuwafutia leseni zao za uagizaji mara
watakapogundulika kutotekeleza maelekezo hayo.
Waziri
Mkuu ametoa onyo hilo leo (Jumatano, Novemba 7, 2018) wakati akizindua
mkakati wa Bunge wa masuala ya kijinsia, Bungeni jijini Dodoma. Amesema
Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha
kuwa wanawake wanawekewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kupiga hatua
zaidi.
Amesema hatua hizo ni pamoja na kuondoa kodi ya  taulio za kike ili kuwezesha 


wanafunzi wa kike ambao walikuwa wanaacha masomo kutokana na changamoto ya 


kununua taulo za kike kwa ajili ya kujisitiri wakati wa hedhi wazipate kwa gharama nafuu.
Waziri Mkuu amesema hatua nyingine ni mpango wa Serikali wa kujenga zahanati kila kijiji


na kituo cha afya katika kila kata kwa lengo la kupunguza vifo vya wanawake na watoto 


vilivyokuwa vinasababishwa na uhaba wa huduma za afya ya mama na mtoto. 
Amesema mpango huo wa Serikali unatarajiwa kuongeza tija kwa wanawake hususan 


katika kuwapunguzia muda ambao wamekuwa wakiutumia katika kutafuta huduma hizo 


ambazo zilikuwa zinapatikana kutoka umbali mrefu.
“Imethibitika
kupitia tafiti za kitaifa na kimataifa kwamba uzazi wa mpango huweza
kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa hadi asilimia 44 na vifo vya
watoto kwa hadi asilimia 35.

 Pamoja
na kulinda afya ya mama na mtoto, huduma hizi zinawasaidia wanawake na
wasichana kupata nafasi za kujiendeleza zaidi pamoja na familia zao na
kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi, kijamii, na
kimaendeleo.”
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuwahamasisha wanafunzi
wa kike kusoma masomo ya sayansi sambamba na kuwawekea mazingira
wezeshi. 
Amesema
hatua nyingine ni mpango wa Serikali wa kuwasomesha wanawake katika
ngazi ya uzamili ili waweze kushika nafasi nyingi zaidi za uongozi
Serikalini na mahali pa kazi. Zoezi hilo linaratibiwa na Idara Kuu ya
Utumishi.
Katika hatua nyingine,Waziri
Mkuu amesema mifumo yetu, mila na historia vimewafanya wanawake na
wasichana wabaki nyuma kwa kujiajiri kwenye sekta isiyo rasmi na isiyo
na kipato cha uhakika wala maslahi na kubaki wakiwa wategemezi
kiuchumi. 
Amesema hivi karibuni Serikali imeanza  kutekeleza kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya 


kumtua mama ndoo kichwani. Kampeni hiyo inalenga kuwaondolea wananchi hususani 


wanawake tatizo la upatikanaji wa haraka wa huduma ya maji safi na salama. 
Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge linaendeshwa kwa


kuzingatia uwiano wa kijinsia kwa kiwango cha kuridhisha. “Hata tunapoteua baadhi ya 


wabunge kwa ajili ya kutuwakilisha katika mikutano mbalimbali huwa tunazingatia uwiano 


wa kijinsia.
Amesema
atahakikisha Bunge linaendeleza azma ya Serikali ya kujenga Taifa lenye
usawa wa kijinsia inatimia, ambapo amewataka mawaziri wanapowasilish
hotuba za makadirio ya mapato na matumizi ya wizara zao waeleze namna
walivyotekeleza jambo hilo.

Share.

About Author

Leave A Reply