Thursday, August 22

WATU MAARUFU KATIKA LEKSIKOGRAFIA YA KIINGEREZA

0


Leksikografia ya kiingereza ina historian ndefu sana , hawa ndio wataalamu maarufu katika uwanja huu.

1. Samweli Johnson
Anaaminiwa kuwa kuwa yeye ndiye aliyeipa leksikografia ya kiingereza umbo na maudhui kama ilivyo hivi sasa.Aliangalia kamusi zilizo tangulia na kuongeza mchango wake

Kamusi aliyotunga iliitwa  Dictionary of English language.

Malengo ya kamusi hii yalikuwa
1. Kuhifadhi msamiati
2.kusanifisha kiingereza kwa kuonesha namna ya kutamka na kudhibiti tahajia ya maneno ili kuepusha vibadala anuwai vya neno moja.

3. Kueleza matumizi sahihi ya maneno.

Johnson alitaka kamusi take iwe na mamlaka juu ya matumizi sahihi ya kiingereza kwani msamiati alio uchagua aliutoa katika vitabu vya waandishi bora

Richard C. Trench
Aliwashawishi chama kitunge kamusi mpya inayozingatia kanuni za kihistoria. Alikosoa kamusi za wakati wake na kudai zilikuwa na mapungufu.
1. Hazikuonesha wazi namna maneno yasivyo tumika
2. Maneno yasiyohusiana hayakuingizwa kwa utaratibu mzuri kwenye kamusi
3. Kamusi hazikuondoa mifano  ya matumizi ya zamani na yasasa ya vidahizo
3. Maana za maneno hazikuwekwa zote kwa ukamilifu
5.sinonimu hazikupangiliwa vizuri
6. Maelezo na maana ya vidahizo yalikuwa marefu mno bila sababu

JAMESE MURRAY
Aliyeuliwa na chama cha isimu kuongoza mradi Wa utungaji Wa kamusi alipewa miaka kumi lakimi alitumia zaidi ya miaka 50
Murray aliwatumia watu waliojitolea kukusanya msamiati mpya  na kuwataka
1.wanakili neno lolote jipya, adimu lazamani au linalotumika kwa namna isiyo ya kawaida.
2.Wanakili muktadha Wa neno linapotumika
3.wapendekeze maana ya neno kulingana na muktadha.

Kamusi yake ilikuwa na malengo

1.kuorotjesha kwa utaratibu wakialfabet msamiati Wa kiingereza
3. Kupatia msamiati huo maneno yanayohusu tahajia, maana, etimolojia, na sentence za mifano na matumizi
3.kuonesha mabadiliko ya tahajia yaneno katika historian take tangu lianze kutumika

4. Kuonesha meneno yote Yakima Sikh yaliyo katika maandishi na mazungumzo , msamiati Wa sayansi, ufundi lahaja, na misimu

Kamusi take iliitwa the Oxford English dictionary.

Noah Webster
Muasisi Wa kamusi za kiingereza cha kimarekani alikiwa mtunga kamusi Wa mwisho iliyokuwa na vitomeo 70000.
Webster alibaini kasoro katika kamusi ya Johnson kama

1. Ilikiwa na taarifa zisizo kuwa sahihi
2.Aliingiza msamiati Wa hadhi ya chini, maneno yaliyokuwa na matusi na maneno ya kilatini

3.Alitua mifano ya matusi kutoka kwa waandishi wasiokuwa wamilisi Wa lugha.
Hivyo akatunga kamusi mpya.

Phillip Give
Yalikuwa mhariri Wa kamusi ya Webster third New international Dictionary.

Gove aliendeleza kanun za leksikografia iliyoanzishwa na Johnson na kufuatwa na Noah Webster na kuendelezwa na Murray.

Shutuma dhidi ya GOVE

1.kamusi iliingiza maneno ya matusi
2.haikuweka mipaka ya matumizi ya baadhi ya maneno

3.haikubainisha matumizi sahihi na potofu ya kiingereza
4.kamusi haikuyumia viashiria vyenye kudhihirisha matumizi potofu

5.Wahakiki waliaminj kuwa madondoo ya kamusi hayana budi kunukuliwa kutoka katika waandishi bora hivyo Gowe alidondoa kwa waandishi waiokuwa bora

Mapitio

J.S. mdee( 2006) nadharia na historia ya leksikografia
www.masshele.blogspot.com

Share.

About Author

Leave A Reply