Friday, July 19

WATEJA WA TIGO SASA WANAWEZA KUFANYA MALIPO KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI WA MALIPO SERIKALINI (GePG)

0


Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed(wa katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu wateja wa Tigo kuanza kufanya malipo kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa malipo Serikalini. (GePG)

Mkuu wa Kitengo cha Biashara
na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya(Kulia)
akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa Habari kuhusu wateja wa Tigo kuanza
kufanya malipo kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa malipo Serikalini.
(GePG)

Bernard Mabagala Afisa Mwandamizi wa TEHAMA – Wizara ya Fedha na
Mipango (kushoto) 
akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa Habari kuhusu wateja wa Tigo kuanza
kufanya malipo kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa malipo Serikalini.
(GePG)

Fanya
malipo ya haraka, urahisi na kwa usalama zaidi kwa zaidi ya idara 300 za serikali,
mawakala na mamlaka za udhibiti kwa Tigo Pesa

29Januari, 2018. Dar es Salaam.  Wateja
wa Kampuni ya Tigo, sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki
wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini
kwenye App yake ya Tigo Pesa.


Akiongea katika uzinduzi wa GePG kwa
mtandao wa Tigo yaliyofanyika  jijini Dar
es Salaam, Bernard Mabagala Afisa Mwandamizi wa TEHAMA – Wizara ya Fedha na
Mipango alisema kuwa ubunifu na juhudi za Serikali katika  kuanzisha mdumo huo wa Kieletronbiki wa
Malipo Serikalini (GePG) umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo
kwa wananchi. Pia imeleta faida nyinginezo ikiwemo kuboresha uwekaji wa
kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza uvuvaji na ubadhirifu pamoja na
kuongeza mapato kwa idara mbali mbali za Serikali. na


Kupitia mfumo wa GePG Serikali pia
imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za
biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza
kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali au kwa
njia mbali mbali za kimtandao, na kufanya malipo ya ankara kwa urahisi na
mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao. 


“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali
ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo na mkakati
wetu,” alisema Hussein Sayed, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kifedha wa Tigo.


“Zaidi ya wateja milioni 7
wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa
haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia
Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Biashara
na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya.


Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo
Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Shirika la Kodi Tanzania (TRA), Shirika la
Umeme Tanzania TANESCO, Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
Mamlaka ya Hifadhi ya Mbuga za Wanyama (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo
ya Makaazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara ya Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya
Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA),
Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile
Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300.


Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo
wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya
siri ili kufanikisha muamala.Ili kufanya malipo kwa kutumia menu ya Tigo Pesa, mteja anatakiwa
kufuata hatua zifuatazo;.


1)     
Kupiga *150*01# kisha kuchagua Lipa Bili

2)     
Kuchagua namba 5 (Malipo ya Serikali)

3)     
Kuingiza tarakimu 12 za mamlaka au taasisi anayotaka
ipokee malipo

4)     
Kuingiza kiasi cha fedha anachotaka kulipa

5)     
Kuingiza namba ya siri kwa ajili ya kuruhusu malipo


Kwa upande mwingine, wateja
wanaweza kutumia App ya Tigo Pesa ambayo inarahisisha ufanyaji wa malipo kwa kiasi
kikubwa.


Baada ya kukamilisha malipo, wateja
wa Tigo watapokea risiti ya kielektoniki kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi
unaothibitisha kuwa muamala umefanyika kikamilifu. Risiti hiyo ya kielektroniki
inakubalika kama uthibitisho tosha wa malipo na inaweza kusaidia kurahisisha
kufuatilia malipo kwa kuwa ni rahisi kuhifadhi na kuipata pale inapohitajika
ukilinganisha na risiti za karatasi ambazo ni rahisi kupotea au kuharibika.


Tigo inawakaribisha wateja wake
kuanza kutumia huduma hii ya Malipo ya Kieletroniki Serikalini (GepG) sasa.


Kuhusu Tigo


MIC Tanzania PLC ni kampuni ya simu
inayoongoza kwa huduma zinazohamasisha maisha ya kidigitali Tanzania. Tigo
ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995. Kupitia bidhaa zake
mbalimbali za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za
kifedha kwenye mitandao ya simu za mikononi; Tigo imekuwa mwanzilishi katika ubunifu
wa kidigitali kama vile simu ya kwanza ya smartphone kwa Kiswahili, huduma ya
Facebook bure kwa lugha ya Kiswahili, App ya TigoPesa, App ya Tigo Mobile
pamoja na huduma ya kwanza Afrika Mashariki ya kutuma fedha kwa njia ya simu za
mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya
nchi husika Afrika Mashariki

.     

Tigo ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini
na kwa miaka mitatu mfululizo, imekuwa kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi
nchini. Kupitia mkakati mkubwa wa kupanua na kuboresha huduma zake, kati ya
mwaka 2015 hadi 2016, Tigo  ilizindua
mtandao wa 4G LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine 22 nchini.


Tigo inajivunia zaidi ya watumiaji milioni
11 wa simu waliosajiliwa, na imetoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zile
zisizokuwa na moja kwa moja kwa Watanzania wapatao 300,000; hii ikiwa ni pamoja
kwa wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia
simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.  


Tigo ni nembo ya kibiashara ya Millicom,
kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya maisha ya kidigitali katika nchi 13
duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za kibiashara katika bara la Afrika na
Amerika ya Kusini, Ofisi kuu za Millicom zipo Ulaya na Marekani.

Kwa
taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz au wasiliana na: 

Woinde
Shisael – Meneja Mawasiliano

Simu:
+255 713 123431            Barua pepe:
Woinde.shisael@tigo.co.tz

Share.

About Author

Leave A Reply