Tuesday, August 20

TFF KUAMUA TIMU ITAKAYOCHEZA NA SEVILLA KATI YA SIMBA NA YANGA

0


<br /> TFF KUAMUA TIMU ITAKAYOCHEZA NA SEVILLA KATI YA SIMBA NA YANGA – MASHELE BLOG<br />


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), ndilo litakaloamua nani akipige na moja ya timu vigogo kutoka nchini Hispania.

Sevilla moja ya timu inayojulikana kwa bora wa soka barani Ulaya na ubebaji wa kombe la Europa League, itakuja nchini mwezi ujao kucheza mchezo mmoja wa kirafiki.

Awali, Kampuni ya Michezo ya Kubeti ya SportPesa inayoileta timu hiyo, iliamua Yanga na Simba zicheze mechi na mshindi acheze dhidi ya Sevilla.

Hata hivyo, ilielezwa ratiba ya Ligi Kuu Bara inayokwenda ukingoni inaonekana kuwa imebana sana. “Kutokana na hali hiyo, tumeambiwa SportPesa wameamua kuwaachia TFF waamue kuhusiana na suala la timu ipi itacheza na Sevilla.

“SportPesa walitaka Yanga na Simba washindane, mshindi basi angepata nafasi hiyo ambayo ni sehemu ya bahati kubwa kucheza na moja ya timu bora duniani.

“Lakini sasa TFF nao wamekubaliana na SportPesa kwamba ratiba imebana, hivyo wameachiwa wao ndio wataamua kama nilivyokudokeza,” kilieleza chanzo.

Sevilla mi moja ya timu zinazotoa ushindani kwenye La Liga na hadi sasa inakamata nafasi ya sita kwenye ligi hiyo ikiwa inapambana kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao


Share.

About Author

Leave A Reply