Monday, August 26

SEVILLA YATUA DAR KUKIPIGA NA SIMBA

0


<br /> SEVILLA YATUA DAR KUKIPIGA NA SIMBA – MASHELE BLOG<br />

Msafara wa wachezaji 18 na viongozi wa Klabu ya Sevilla FC umetua nchini saa 1:40 usiku wa leo.

Sevilla wametua nchini chini ya uratibu wa Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa pamoja na Laliga.

Sevilla wakiwa hapa nchini watacheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Simba kesho kutwa Alhamisi utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya Sevilla kutua, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas amesema kuwa anafurahia ujio wa Sevilla ambao utaongeza utalii nchini.

Tarimba aliwatahadharisha Sevilla kwa kuwaambia kuwa wajiandae wanacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

“Ninawaambia kuwa jiandaeni kupambana na mabingwa wa ligi hapa nchini ambao ni Simba.

” Ni timu nzuri iliyojiandaa kuhakikisha inapata ushindi kutokana na ubingwa walioupata,”amesema Tarimba.


Share.

About Author

Leave A Reply