Sunday, August 18

RC AWAKUTANISHA VIONGOZI NA WATAALAMU KATIKA KIKAO CHA MAJUMUISHO YA ZIARA DAR

0


*Awapongeza watendaji kwa kuufanya Mkoa huo kuwa kinara ukusanyaji mapato
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanya kikao cha majumuisho
kilichowakutanisha wakuu wa Wilaya, wakurugenzi, wakuu wa Wilaya,
Makatibu Tawala, washauri wa miradi na wakandarasi na hiyo ni kufuatia
ziara iliyofanywa na RC huyo katika kukagua miradi mbalimbali ya
kimaendeleo jijini humo.
Akizungumza
na watendaji hao Makonda amewapongeza watendaji kwa juhudi
wanazozifanya katika kuleta maendeleo na kuwataka watimize ahadi zao
kama walivyohaidi na hiyo hasa ni katika ujenzi wa vituo vya afya
Buguruni na Kigogo kwa kuikamilisha kwa wakati huku akifurahishwa na
kasi ya ujenzi wa hospitali za Wilaya za Ilala na Kigamboni ambazo
zinajengwa kwa jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha ambazo zilizotolewa
na Rais John Joseph Magufuli katika kuboresha sekta ya afya.
Aidha
ameitaka Halmashauri ya Ubungo kuongeza kasi zaidi katika utatuzi wa
kero za wananchi na kuwataka viongozi kuacha siasa na kuchapa kazi huku
akielekeza nguvu zaidi iwekwe katika  shughuli za kimaendeleo.
Vilevile
amewasisistiza wataalamu wa kusimamia miradi jijini humo kushirikisha
wazawa katika miradi mikubwa ya kimaendeleo pindi tenda zinapotangazwa
ili kuweza kuwainua na kuwapa fursa zaidi.
Wakati
huo huo Makonda ametumia nafasi hiyo kuzipongeza halmashauri zote na
watendaji wao kwa kuufanya Mkoa huo kuwa kinara katika ukusanyaji wa
mapato kwa kipindi cha robo mwaka kwa kukusanya zaidi ya shilingi
bilioni 118.4 ikifuatiwa na Jiji la Dodoma lililokusanya  bilioni 57.3
na Jiji la Mwanza shilingi bilioni 22.9 huku Wilaya za Ilala na
Kinondoni zikifanya vizuri zaidi nchini.
Ziara
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ilimulika miradi mbalimbali ya
kimaendeleo katika Wilaya zote jijini humo na katika ufanyaji wa
tathimini hiyo viongozi na wasimamizi wa miradi hiyo wametakiwa kutimiza
ahadi zao kwa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Share.

About Author

Leave A Reply