Friday, July 19

RAIS DKT MAGUFULI NA UHURU KENYATA KUZINDUA KITUO CHA FORODHA CHA PAMOJA KESHO

0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta walipokutana leo kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC)  leo Novemba 30, 2018 (Picha na Ikulu)

Na Vero Ignatus, Arusha
RAIS 
Dkt John Magufuli na Rais Uhuru Kenyata  kesho wanatarajia kuzinduwa
kituo cha Forodha cha pamoja Namanga One Stop Bonder Point.
Aidha
Disemba 2,  mwaka huu Rais John Magufuli ataweka jiwe la Msingi la
mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh bilioni 520  katika Jiji la
Arusha na baadhi ya maeneo katika wilaya ya Arumeru.


Taarifa
hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo alisema
kituo hicho cha Forodha kimejengwa kwa ushirikiano wa nchi ya Kenya na
Tanzania. Kwa mujibu wa Gambo kituo hicho cha forodha kitakuwa
mwarobaini wa kubithibiti vichochoro vya kupitisha magendo zikiwemo
nyara za serikali.
Alisema katika kuimarisha ulinzi wa kituo hicho
mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Saimon Sirro ametoa mbwa wawili ambao
watagundua aina yeyote ya magendo ikiwemo meno ya tembo,madawa ya
kulevya na mlipuko.


“Niwasihi
wananchi wote kuheshimu sheria za nchi kwa kuepuka kufanya vitendo vya
kupitisha magendo kwenye mpaka wa Namanga kwa kuwa vyombo vya ulinzi na
usalama vimeimarisha ulinzi na watakaobainika watachukuliwa hatua kali
za kisheria.
Kuhusu uwekaji msingi mradi huo wa maji Gambo alisema
Rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi eneo la chanzo cha maji hayo
kilichopo wilayani Arumeru.Alisema baada ya kuweka jiwe hilo la Msingi
atatembelea ujenzi mradi huo kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha
sambamba na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Share.

About Author

Leave A Reply