Thursday, August 22

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA WIMBO WA KIJALUO

0


Mwandishi,
Happines

Iks/UDSM

Jina la wimbo

Milly Nyarjolang’o
Ohh Milly mamii
Onyango wuod Odhiambo ka koro atugo duma jey ma minoken x2 Paro chanda Onyango warire chien, nyakaocha toti aere ngima, Iwuonda nang’o, mami kiri wuonda jaber. Nyarjodongo toti nyathi jalang’o kionge chiemo tama nang’o. Oluora, oluoro mine na, oluoro wuone na, ni koda yuoche na. Jodongo donge opwoyo ni nyarmasai oromo dak, chieng ukowa nywomo. Kenn Agola osiepa nukowa nywomo, kondakta Otieno nu kowa nywomo, Otieno wuod osiri x2
Nyathi marwakona gwen ma kata aonge dala, suba to nyieranyiera, ana donjo dala Milly romo naa, ne wanyiedho kode, to ne wagoyo mbaka. Adundo oting’o chak ana golo yier e’chak x2. 


Nyarjalang’o toti nyathi jalang’o wapuro godo kane wadok dala to Milly omako kweru to jasuba sembo dhok ni yuor Akenn jangoma, yuor Ajoji, Joji nyangoma yuor Ogutu panga lili baibai.
Ben wuod Odhiambo atugra omina Aoko, wuod Adhiambo atugra to ma to wer chieng’ orana nono papa x2. Wuololo Onyango ja waya atug thuma. Sama wero Amilly nyajalang’o ni yuor Ajoji ma nyako to inemara. Jothum ma sani wero mana mon to ma gibayo go. Anawero chiegaaaaa, Milly nya jalang’o aero ka nanga na ma umo duga, oera ka ero ngima na oyuor Ogutu.
Kanadonjo dala jathum odenyo Amilly tedona, juogi oramo dwaro lang’o Atieno atim nang’o, ken x2 ochuna  ating’o punde wuod adhiambo adonjo tanga dala kadhi manya Amilly mamaaa x2. Adonjo tanga dala, papa adonjo Mara dhi manyo nyathi masai na, akalo korotambe i-onge, akalo Iramba thur ga Geng’o i-onge, Ageng’o ja Iramba no rwako ya. Jaote wuod Akelo no rwako ya.
Achopo nyang’ombe dala thur ga molo. Nyiri mane miela e mana yiere happy na, aluongo nyarjalang’o bi nee x2. Milly biro gi mwoloooo kako ong’eyo chike lang’o, nyako ogik to mosa gi luor, toti iber na, chonge ogona piny, okona Odhiambo wuod Adhiambo papa ana eri, kanyo e mane wawinjoree e mane wakendoree
Awuok Tanga, Onyango adonjo Kenya gi nyako e kinda koda Amilly, Ruoth osegwedhowa wan gi Tonny mama. Obera nyarjolang’o to paro chieng’ nega nono sama wero marita, Milly e-matedo na wuololooo nyar jalang’o nyathi masai naaa x2
Akao Milly na atero dalawa, kanawuok dala wa, kanadhi kamenyo, kanaduogo dalawaaa. Minwa bende romo na gi mor, to mama kwodho na, Milly nyarjolang’o mama nyathi masai oromo dak x2. Omora Onyango ja lamo maduogo aleng’oraa.
Wuololooo Onyango ja’wer, chonga nego nanga, Ni josem rulo ko rwako wuoche akala semga x2 ne gikone  Onyango okinyal dak go negikoni papa jey okinyal dakgo gi madwogo koro wuod adhiambo ni Milly nyar’jolango okwero jogo ni oknyalre, chwora ni taere e ngima na emanadak go, piny kakarambo onge maskini. 


Nyajalang’o mama, Amilly mama x2
Mon mabeyo aneno adii, nyiri maber aneno tee, mon mabeyo aneno tee, to mago aweyo tee nikech inemasingorekodi, kaponi akwongo ni to iniywaga x2, to kaponi ikwongo na jaber to atim nade mama to maina, Happy aero ka nanga. Nyathi gi’ jaki, nyathi gi’Milly nyalang’o
Jaber nyarjalang’o awei gi mago to wananere, aneno timbe ne imora gi madaga ayiego. Uzuri wa mke si urembo, uzuri wa mke ni tabia, aparo Milly nyarjolang’o nyathi masai.

Tuishi na mani na mwenzako kati yangu na Milly, utulivu tele kati yetu.
Maelezo kuhusu wimbo.

Wimbo huu umeimbwa na mwanamuziki wa kizazi kipya wa Kenya anayeitwa Benn Odhiambo kwa jina maarufu Onyi papa j.

Wimbo huu ulitoka na kuanza kupigwa katika vyombo vya habari nchini Kenya na mpakani mwa Kenya na Tanzania kwani ndipo wazawa wa lugha ya kiluo wapo mfano maeneo kama Tarime, Rorya, Musoma, Bunda na Serengeti,
Msanii katika wimbo huu, aliutunga kwa kusudi maalumu la kumuimbia mke wake ambaye ni mwanamke aliyeitwa Milly kutoka jamii ya kimasai (lang’o).

Ameimba tangu alivyomtafuta na kumpata ndipo alipomuoa na kumpeleka Kenya kwa mama yake, wazazi na ndugu wote wa mwanaume walimkubali Milly kuwa ni mwanamke anaye faa kuolewa.

Msanii kupitia wimbo huu, japo amemuimba mke wake lakini katika uchambuzi amemsawiri mwanamke kwa namna tofauti tofauti, mathalani amemsawiri mwanamke kama mtu muhimu sana katika ndoa kwani bila mwanamke hakuna ndoa, amemsawiri pia kama mama mfano mama yake mzazi na mke wake, pia kwa namna nyingine amemsawiri mwanamke kama chombo cha starehe yaani mstareheshaji mfano alivyowaimba wanawake waliokuwa wakicheza mbele za wanaume na kuwafurahisha pia alivyoeleza jinsi wasanii wanavyo imba mahawara pasipo kuwaimba wakezao.

Katika makala hii  tumeigawa katika sehemu tatu yaani utangulizi, kiini na hitimisho.

 Katika utangulizi tumeeleza dhana ya nyimbo kupitia wataalamu mbalimbali na maana ya usawiri wa mwanamke katika kazi za fasihi. Katika kiini tumeangalia namna mwanamke anavyosawiriwa katika wimbo wa kiluo wa “Milly nyarjolang’o” ulioimbwa na msanii Onyii Papa J kutoka Kenya na katika hitimisho tumehitimisha kwa kutoa maoni juu ya usawiri huo.

Balisidya (1987), anasema kuwa nyimbo ni tungo za kishairi zenye kutumia mahadhi, melodia, mkong’osio, mapigo na muwala. Hivyo kwa ufupi nyimbo ni tungo ya kishairi yenye mpangilio maalumu. Vilevile na Ngure (2003), anasema nyimbo ni kama tungo iliyo na mahadhi ama mdundo na unaoweza kuimbika.

Anaendelea kusema kuwa kupiti a nyimbo jamii inajifunza, inacheka, inafarijika inapeana moyo na kupitisha taarifa za siri.

Pia Mutua na Munywoki (2011) wanafasili nyimbo kuwa ni aina ya sanaa katika fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti ya kiimbo maalumu, aghalabu nyimbo hutumia ala za muziki kama vile ngoma. Wanaendelea kufafanua kuwa nyimbo zinaweza kuimbwa na mtu mmoja au zaidi na nyimbo nyingi huwa na kiitikio au mstari ambao hurudiwa rudiwa.
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa nyimbo ni tungo zenye mahadhi ya sauti inayopanda  na kushuka na tungo hizi huundwa kwa lugha ya mkato, matumizi ya picha na mapigo ya silabi na hupangwa kwa utaratibu wenye mapigo ya kimuziki.

Wamitila (2010) anasema kuwa usafiri ni hali na mtindo wa uwasilishaji wa wahusika, mandhari na matukio katika kazi ya kifasihi. Wataalamu mbalimbali kupitia kazi zao za kifasihi yaani fasihi andishi na fasihi simulizi wamemsawiri mwanamke kwa namna mbalimbali mathalani Matteru (1982), ambaye amechunguza suala la mwanamke katika fasihi simulizi ya Tanzania, anaeleza kuwa taswira ya mwanamke inayojitokeza katika vipera vingi vya fasihi simulizi ni ile inayomuonesha kuwa ni mama wa nyumbani, chombo cha starehe na bidhaa.

 Mawazo ya Matteru (1982) yanatupa mwanga juu ya usawiri wa mwanamke katika kazi za fasihi simulizi kama alivyobainisha, hata hivyo kwa ujumla kazi hii pia itachunguza taswira ya mwanamke iliyojitokeza zaidi katika wimbo wa kiluo kutoka kwa msanii Onyii Papa J kama kipera mojawapo cha fasihi simulizi.

Kwanza, mwanamke ni mpenda starehe, suala hili limejitokeza katika kazi nyingi za fasihi ya kiswahili. Lyatuu (2011) anaeleza kuwa mwanamke anaonekana kuwa ni kiumbe ambaye anapenda kupata starehe kwa gharama za wanaume na si zake yeye binafsi, hatahivyo mwanamke hawezi kufanya starehe pekeyake, hushirikiana na mwanaume katika starehe kwani wanaume ndio huwafata wanawake kushiriki nao katika starehe.

 Siku zote katika jamii ya mfumo dume mwanamke ndiye husukumiwa mabaya yote. Katika wimbo huu wa kiluo wanawake wametumiwa kama wastehereshaji wa sherehe nyakati za usiku kwa kuchukuliwa na wanaume na kucheza nao. Msanii anaeleza kuwa wakati alipoenda kumtafuta mke wake alimpata miongoni mwa wanawake waliokuwa wakiwachezea na wakapendana tangu hapo.

 Mathalani”Achopo nyang’ombe dala thur ga molo, nyiri mane miela e’mana yiere happy na,  aluongo nyar jalang’o bine”….x2
Tafsiri; Nilipofika nyumbani Nyang’ombe kwao Amolo, miongoni mwa wasichana waliokuwa wakituchezea ndipo mlipomchagua hepi  wangu
Vilevile katika wimbo huu mwanamke anaoneshwa namna wanavyowatumia katika uzinzi, msani ameimba kuwa yeye anamuimba mke wake tofauti na wanamuziki wengine wanaowaimba wanawake wanaotembea nao yaani wanaokuwa nao katika mahusiano ya kiampenzi na sio wakezao, dondoo hii inaonesha kuwa wanaume waliooa hutoka  nje ya ndoa na wanawake wengine ambao yawezekana wameolewa au hawajaolewa, hivyo bado mwanamke anaonekana kama chombo cha starehe.

Mathalan
“jo thumbe masani wero mana mon to ma gibayo go x2…anawero chiegaaaa, Milly nyajolang’o aero ka nanga na maumo duga, oera kaero nyaroya omina Atieno..”
Tafsiri;  “wanamuziki wa sasa wanawaimba tu wanawake wanaotembeanao na si wake zao, ila mimi namuimbia mke wangu. Milly mtoto wa kimasai nampenda kama navyoipenda nguo yangu inayonifunika uchi”

Hivyo basi, dhana ambayo watu wamejiwekea kwa kuwa mwanamke ni mtu anayependa starehe ni potofu kwani starehe haifanywi na mwanamke tu, starehe inajumuisha mwanaume na nwanamke hasa mwanaume ndiye mshawishi mkubwa kwa mwanamke.

Pili, mwanamke ni kiumbe mchapakazi, wanawake ndiyo wafanyakazi wakubwa wakutumainiwa katika shughuli za kilimo, ufugaji na ufanyaji wa shughuli ndogondogo za ndani kama kupika, kuosha vyombo na kazi zote za nyumbani vilevile wasanii wengi wamemsawiri mwanamke kama mchapakazi wa kazi za nyumbani  na za ujasiriamamli  Mbogo (2002), anamwelezea Kurwa kuwa anapenda kazi, alifuatana na Maman’tilie kwenda gengeni, huko alimsaidia kuuza chakula. Hata siku moja kurwa hakuchoka kufanya kazi. Vile vile na katIka  wimbo huu mwanamke anaonesha namna alivyokuwa mchapakazi na msaidizi wa mume wake katika kazi kama kilimo na ufugaji. Mfano;
“Nyathi ma rwako na gwen ma kata aonge dala, Suba to nyieranyier. Anadonjo dala Milly romo na ….., ne wanyiedho kode to ne wagoyo mbaka…..  Nyarjalang’o toti nyathi ja lang’o wapuro godo kane wadok dala to Milly omako kweru ti jasuba sembo dhok”
Tafsiri; Mtoto anayeniingizia kuku ndani mimi nimekaa tu nafurahia, nikija ananipokea, tunakamua maziwa wote…..mtoto wa kimasai toti, mtoto wa kimasai tulilima nae, tulipokuwa tukirudi nyumbani kutoka shambani alishika jembe mimi nilipiga ng’ombe kuelekea nyumbani.
Hivyo, mwanamke anasawiriwa kuwa mchapakazi wa shughuli za uzalishaji mali. Jambo hili limeonekana hata katika jamii ya sasa wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi za kuingiza kipato kwa familia na taifa kwa ujumla, hivyo uwajibikaji wa mwanamke hulinda heshima yake kwani anakuwa sio tegemezi tena kwa mwanaume.

Tatu, mwanamke ni kiumbe wa nyumbani, dhana hii inaaminiwa sana na jamii nyingi za  Kiafrika hasa jamii ya Kiluo. Mwaipopo (1990), anasema kuwa mwanamke hutakiwa kukaa nyumbani akifanya shughuli na mwanaume hutakiwa kwenda kazini kutafuta riziki. Dhana hii pia imeonekana katika wimbo huu baada ya Onyango kumuoa mkewake na kumpeleka nyumbani kwao yaani kwao mwanaume au ukweni na kumuacha kisha yeye akasafiri kwenda mbali kazini kutafuta riziki.
Mfano: “akao Milly na atero dala waa, kana wuok dala wa kadhi emenyo…kanaduogo dala wa minwa bende romo na gi mor, to mama kwodho na….”
Tafsiri; Nilimchukua Milly wangu nikampeleka nyumbani kwetu, nilipokuwa naondoka kwenda kutafuta riziki ..”
Hivyo basi, mtazamo wa jamii kuona wanawake kama kiumbe wa nyumbani mtazamo huu ni hasi, kwani mwanamke naye kama mmoja wa wanajamii anahaki ya kutoka kama mwanaume kwenda kutafuta riziki na sio tu kukaa nyumbani kama mnyama wa kufugwa. Hata hivyo haya yote yanatokana na wivu wa wanaume kwa wakezao na nikwasababu wanafikra na dhana ya udhaifu wa mwanamke kuwa ni kiumbe dhaifu anayeweza kushawishiwa na wanaume wengine hivyo wanawaweka kuwa watu wa nyumbani tu.

Nne, mwanamke ni mama, mlezi na mwangalizi wa familia, kama ilivyodesturi ya watu hasa wa mfumo dume, wanaamini kuwa mama ndiye mtu pekee ambaye ni mlezi wa mtoto na ndiye huwa karibu na mtoto kwa muda mwingi. Suala la malezi limezungumziwa sana na wasanii wa kazi nyingi za fasihi mfano  Mbogo (2002) katika  “Riwaya ya mama’ntilie” amemsawiri mwanamke kama Mama mlezi na mwangalizi mkuu wa familia. Maman’tilie ndiye aliyejua familia yake ile nini, ifanye nini na iishi vipi. Mumewe mzee Lomolomo hakuwa na mchango wowote. vivyohivyo na katika wimbo huu msanii anaimba na kumsawiri mkewake pamoja na mama yake mzazi kama walezi bila kumtaja baba yake mzazi ingawa hatuwezi kujua baba yake yuko hai au ni marehemu. Mfano;

 “kaduogo dala wa, minwa bende romo na gimor to mama kwodho na Milly nyarjolang’o mamaa nyathi masai oromodak, Amilly nyajolang’o nyathi masai oromo dak.
Tafsiri; “niliporudi nyumbani kwetu, mama yangubalinipokea kwa furaha, akaninong’oneza kuwa mke wangu Milly mtoto wa kimasai ni mke anayeweza kukaa na wewe”
Hivyo, kutokana na dondoo hiyo inaonesha namna gani mama wa msanii, alivyo na jukumu la kulea kwani mwanaye alipoondoka kwenda kutafuta riziki alimuacha mke wake,  mama huyo aliishi nae kama mtoto wake na ndipo alimsoma tabia na kugundua kuwa mke wa kijana wake anatabia nzuri na anaweza kuishi na mtoto wake.

Vilevile mke wa msanii alikuwa pia tayari ana mtoto anayeitwa Tonny na alimpa malezi kama mama wakati mumewe alipokuwa mbali akitafuta riziki. Si jambo baya mwanamke kuwa mlezi wa familia lakini kuna haja ya kushirikiana kwa wazazi wote wawili ili familia ipate malezi sawa ya baba na mama.

Tano, mwanamke ni kiumbe mtiifu, mwanamke  ni kiumbe anayetazamiwa kuwa mtiifu kwa wazazi wake, wazazi wa mume wake na hata mme wake na hii hutokana na mfumo dume uliopo katika jamii nyingi mathalani katika kazi  mbalimbali za fasihi wasanii wamemsawiri mwanamke kama kiumbe mtiifu mfano Kezilahabi (1971) katika Rosa Mistika, pale alipomsawiri Regina mama yake Rosa Mistika kuwa ni mtiifu wa hali ya juu kwa mumewe. Mama huyu humtii mumewe kwa kuongea nae kwa ukarimu, upole na unyenyekevu na hapendi kumuudhi.
Vilevile imani za kidini nazo zinasababisha mwanamke kuzidi kuwa mtiifu hasa kwa mwanaume mfano katika Biblia takatifu Waefeso 5:24-25 linalosema ” lakini kama kanisa limtiivyo kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Dondoo hii ni kichocheo kikubwa katika utiifu wa mwanamke hasa kwa wanawake walioshika dini yaani mkristo aliyeamini.

Vivyo hivyo na  katika wimbo huu, msanii anaonesha namna mke wake Milly anavyo mtii yeye, wazazi wake na mashemeji zake, pia alipokuwa katika harakati za kumtafuta Milly alipomuona alimuita na Milly alikuja kwa unyenyekevu na kumsalimia akiwa amepiga magoti. Mfano;
“oluora, oluoro mine na, oluoro wuone na gi koda yuoche ne. Jodongo dongo pwoyo ni nyamasai oromo dak”
Tafsiri ; Ananiheshimu, anawaheshimu mama zangu, anawaheshimu baba zangu na mashemeji zake. Wazee wanasema mtoto wa kimasai ananifaa”
Pia; “Milly biroo gi mwolo, kakong’eyo chike lang’o. Nyako ogik to mosa gi luor….toti iber na, chonge ogona piny”
Tafsiri; Milly anakuja kwa unyenyekevu, kama anavyozijua desturi za kimasai. Alifika na kunisalimia kwa woga, mtoto we ni mzuri huku akiwa amepiga magoti chini.”
Hivyo suala la utiifu wa mwanamke ni zuri lakini likiwa na kiasi, ni kweli kuwa katia maisha ya sasa kupata mwanamke mtiifu na mnyenyekevu kama Milly ni vigumu, hii ni kwasababu nyakati hizi wanawake wameshituka na kuanza harakati za kudai haki zao pale wanapoona wanaonewa na kukandamizwa kwasababu ya unyenyekevu wao, basi na wao hupinga dhana hiyo kwakuiona kama dhana kandamizi.

Mwisho, mwanamke ni mtu mwenye msimamo na mwenye mapenzi ya kweli,  Mwanamke katika kazi mbalimbali anasawiriwa kuwa ni mtu mwenye mapenzi ya kweli na msimamo. Mathalani Mtobwa (1984) anasema kuwa wapo wanawake wachache ambao wana moyo wa kuridhika, usioyumbishwa na tamaa za dunia ambazo mara nyingi huhatarisha usalama wa ndoa zao. Jambo ambalo ni adimu katika kipindi hiki.
Vilevile msanii katika wimbo huu anamsawiri mke wake alivyo na mapenzi ya dhati kwake kwani alipoondoka kwenda kutafuta riziki, wanaume wengine walikuja kumshawishi aachane na mume wake ambae hana pesa, lakini Milly aliwakata na kusema kuwa hapa duniani hakuna maskini.

Mfano; “Milly nyarjolang’o okwero jogo ni oknyalre, chwora ni taere ngima na, emana dakgo. Piny ni onge masikini”
Tafsiri; Milly mtoto wa kimasai aliwakataa na kusema kuwa haiwezekani, mume wangu huyu na mpenda maisha yote na ndiye nitaishi naye kwani ulimwengu huu hauna masikini.
Usawiri huu unampa mwanamke hadhi kubwa, kwani anaonekana kuwa mwaminifu na mzalendo katika mapezi, suala ambalo ni changamoto kwa jinsia zote yaani mwanamke na mwanaume.

Kwa kuhitimisha, tunaweza kusema kuwa wimbo huu wa Kiluo umemsawiri mwanamke kwa mambo hasi na vilevile kwa mambo chanya. Jamii nyingi kutokana na mila na desturi zimekuwa zikimuweka mwanamke chini ya mwanaume. Hivyo jamii zote zinapaswa zibadilike na kuondokana na mtazamo hasi kwa mwanamke.
Marejeleo
Biblia takatifu waefeso 5:24-25
Balisidya, M.L (1987) “Tanzu za Fasihi Simulizi”, Mulika Na 19, Chuo Kikuu cha
                                        Dar es Salaam: TUKI
Kezilahabi, E. (1971), Rosa Mistika. Nairobi: EALB
Lyatuu, J. (2011), ” Usawiri wa Mwanamke Katika Fasihi ya Kiswahili: Ulinganifu wa wa
                                      Waandishi wa Kike na Kiume Uchunguzi Katika Riwaya Teule”.    
                                      Tasnifu ya M.A. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (haijachapishwa)
Matteru, B.M.L. (1982), “The Image of Women in Tanzania Oral Literature: A survey”
                                         Katika Jarida la Kiswahili la TUKI, juzuu Na. 49/2 uk. 1-34.
                                        Dar  es Salaam: TUKI, Dar es Salaam.
Mboga,  E. (2002), Watoto wa Mama’ntilie, Dar es Salaam: Help Publishers
Mutua, M & Munywoki, C.B. (2011). Fasihi Simulizi Katika Kiswahili Gafkosoft.com,
                                                 imesomwa 10/12/2018.
Mtobwa, B (1984), Pesa Zako Zinanuka.  Dar es Salaam, Heko Publishing

Mwaipopo, R. N. G. (1990). “The Impact of Commodity Relations on the Role and Status
                                              of Women in Peasant Households: A Case Study of Rungwe
                                                District”, M.A Thesis, University of Dar es Salaam, Tanzania
Ngure, A (2003) Fasihi Simulizi Katika Shule za Sekondari, Nairobi:Phoenix
                                                 Publishers Ltd.
Wamitila, K. W. (2010), Kamusi Pevu ya Kiswahili. Nairobi: Vide~Muwa Publishers Ltd.

Share.

About Author

Leave A Reply