Monday, August 26

LUGHA KIENZO YA KAMUSI NA FAIDA ZAKE

0


Karibu katika makala haya ambayo tutatalii maana ya lugha kienzo ya kamusi.

Mtunga kamusi anapoazimia kutunga kamusi, anakabiliwa na maswali kadhaa. Miongoni mwayo ni
1. Leksimu zipi ziteuliwe kuwa vidahizo.
2. Taarifa gani zitolewe kwa kila kitomeo ili kukidhi haja ya watumiaji Wa kamusi na
3.  Taarifa hizo zielezwe vipi ili msomaji aweze kuziona na kuzielewa.

Maana ya lugha kienzo.
Lugha kienzo kama asemavyo Bwege (1995) ni lugha au mtindo utumikao kufasili au kueleza leksimu za lugha.
Kwa ufupi lugha kienzo ni lugha inayotumika kuifafanua na kuifasili lugha.
Lugha kama chombo cha mawasiliano imekuwa ikitumiwa kuelezea maarifa, na mambo mbalimbali. Kwamfano lugha hutumiwa kueleza na kufafanua dhana anuwai za hesabu, sayansi, uchumi, ufundi, fasihi nk. Dhima ya lugha kienzo kwa mujibu Wa Bwege ni kueleza lugha kwa ufasaha, utoshevu, kwa muktasari na uwazi ili kumwezesha mtumiaji, kupata na kuelewa mara moja kile anacho kifafanua bila kuchosha akili.

Kamusi kama kitabu cha lugha nacho INA lugha inayotumia kueleza taarifa mbalimbali, zinazohusu kidahizo ambazo huingizwa katika kamusi. Maelezo yanayo ingizwa katika vidahizo ili kukifahamu ni ya kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia, kisemantiki, kietmolojia, na kimtindo.

Bwege(1995 ) lugha hii ni mahususi kwa kamusi na hueleweka tuu inapotumiwa katika kamusi.
Hii ndio huitwa lugha kienzo ya kamusi.

Lugha kienzo ya kamusi.
Lugha kienzo ya kamusi ni lugha ya mjazo au msimbo inayotumiwa kueleza vidahizo katika kamusi( Mdee1992) lugha huu ndiyo anayotumia mtunga kamusi kutoa maelezo ya kisarufi, na kimaana ya vidahizo, maelezo hayo ambayo  mtumiaji Wa kamusi huyafuata anapoirejelea kamusi. Ili lugha kienzo iweze kuwa faafu kwa msomaji Wa kamusi hainabudi kuwa sanifu, rahisi na yenye kueleweka.

Mapitio
www.masshele.blogspot.com
Mdee(2010) Nadharia na historia ya leksikografia.TUKI: Dar es salaam.

Share.

About Author

Leave A Reply