Saturday, August 24

KIONJO CHA RIWAYA: CHRISTINA

0


Mtunzi
info.masshele@gmail.com

..Mle ndani ukimya ulitawala na mazungumzo yaneno moja moja yalikuwa yakiiba nafasi ya ukimya uliokuwopo, kila mtu aliwaza lake, wenye kuhuzunika walihuzunika, walio mhurumia Christina nao walipata mudahuo wa uchungu. Kitanda nacho kiliumia kwa upande wake! Licha ya kubeba mwili dhaifu wa Christina , watu wengine walikaa wakimtazama Christina kwa huruma. Hawa sio wengine bali ndugu wa Christina.
…. Mgonjwa, ugonjwa umemlemea kila kiungo ni kizito. Mama Christina anajaribu kumnywesha mgonjwa uji lakini wapi! Uji hauendi umejaa mdomoni kisha unachuruzika unatoka koo halifunguki Ugonjwa umemzidiya. Glory anachukua kitambaa anamfuta mgonjwa jasho lenye harufu kali ya antibiotics, dawa ambazo nazo zilikuwa zimeanza kufika mwisho.
Christina anajaribu kuwatazama watu waliokuwa pale , kwanza mama yake lakini hammalizi anaangalia pembeni. Anamtazama Glory naye hammalizi pia anaamua kutazama ukutazama pembeni. Anaona aibu mara hii katika kumalizia mda wake mchache uliobaki.
Christina anatamani kusema. Ulimi unasema hapana umekuwa Mzito! Anatamani kusema kwaheri Mama lakini neno halimtoki! , hana nafasi hiyo tena.
Kila mtu anamhurumia! Kwanamna ambavyo hatii matumaini.
Kifo kilikuwa kinakaribia tayari kuahirisha safari ya Christina. Kilikuwa kinakwamisha tayari ndoto zake!! hata zile nguona Vito kadha wa kadha alivyokuwa amepanga kwajili ya Harusi yake zilikuwa kazi bure! Malaika mtoa Roho tayari na Christina alianza kuhisi harufu yake ndio maana alianza kuhangaika hadi kutia tone la tumaini. Malaika mwenye zamu sikuhiyo tayari alisogea na Bakuli lake!

Katika ulimwengu wa nafsi Christina alianza kuwaona wazee na wahenga wake! walikuwa hawana furaha! walikuwa hawako tayari kumpokea Christina,  sura zao zilizidi kumtia hofu hali hii ilimfanya atokwe na machozi yaliyotirika katika mashavu yake katika mwili halisi.
Kunakitu anakiona alisema mama Christina huku na yeye akitokwa na machozi. Upendo wa mama humhurumia mwanae hata kama Mwana kajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe.
Mara gafla Christina alianza Ku……………..
Itaendelea?

Share.

About Author

Leave A Reply