Sunday, August 25

HISTORIA YA KAMUSI

0Historia ya kamusi ilianza katika jamii zilizojua kusoma na kuandika. Kamusi ilihitaji imsaidie mtumiaji kufahamu maana za maneno aliyo yasoma au kuyasikia lakini hafahamu maana zake. Maneno hayo yalipatikana katika matini matini mbalimbali. Kwa hali hii haja ya kamusi ilichochewa kwa maendeleo ya lugha na kupanuka kwake. Orodha ya meneno magumu iliyo kusanywa kutoka katika matini fulani na kutolewa maelezo, ya maana za maneno hayo iliitwa Faharasa.

Mwanzo Wa kamusi ni Faharasa.
matini ya mwanzo ambayo inafikiriwa kuwa ni kamusi ya kwanza ilikiwa ya kisumeri-kiakadi , hizi zilikuwa lugha za mesopotamia katika nchi ya Iraki ya Leo. Wasumeri walioishi Mesopotamia ya kisini walikiwa watu waliostaarabika sana miaka 4000-2000 kabla ya yesu. Wakati Wa ustawi Wa dola yao waligundua maarifa anuwai.hesabu na hifadhi ya nyaraka na namna ya kuandika.
Na maarifa yao mengi yaliandikwa katika matofali mabichi ya mfinyanzi . baada ya utawala wao kuangushwa na waakadi Wa mesopotamia ya kaskazini miaka kama 2350KK, Kisumeri kiliendelea kutumiwa na waakadi kama lugha ya elimu. Waakadi walijifunza kisumeri ili waweze kusoma katika taasisi za wasumeri . Ili kuwasaidia wanafunzi Wa lugha ya kisumeri msamiati Wa kisumeri  uliorodheshwa pamoja na visawe vyake katika lugha ya Kiakadi (Mc Arthur1986)
 Baadaye hali hii ya kukusanya msamiati iliendelea katika ,uchina , ugiriki, uingereza ,urusi

Faharasa ya Kingereza

*Kamusi ya maneno magumu. Inadaiwa kuwa wanazuoni waliandika maana za maneno ndani ya vitabu walivyo visoma ambayo baadaye yalikusanywa na kufanywa Faharasa ya kilatini-kiingereza.

Aina za Kamusi

1.kamusi ya lugha mbili iliyoanza kuandika  , Thaniya
2. Kamusi ya lugha moja wahidia

3. Kamusi ya lugha zaidi ya mbili , Mahuluti.

Faida za Kamusi
1. Kueleza namna neno linavyo andikwa , tamkwa nk
2. Kusanifisha lugha
3. Kuhifadhi maneno
4. Kujifunzia lugha, utamaduni na maarifa.

Itaendelea
J. S. Mdee(2006) nadharia na historian ya leksikografia.
www.masshele.blogspot.com

Share.

About Author

Leave A Reply