Wednesday, August 21

HISTORIA NA MAENDELEO YA RIWAYA YA KISWAHILI

0


Kabla ya kuelezea historia na maendeleo ya riwaya ya Kiswahili ni vizuri kujua mambo machache katika kuelezea historia ya riwaya ya Kiswahili kabla ya kujibu swali.
Mambo ambayo yanafungamana na chimbuko la riwaya ya Kiswahili ni nini maana ya riwaya, riwaya Kiswahili ni ipi, ukubwa wa riwaya, ugumu au wepesi wa riwaya.

Riwaya ni utanzu mmojawapo tu kati ya tanzu za fasihi andishi ambazo hujumuisha tamthiliya, hadithi na ushairi (mkacha na madumulla, 1991:1).

 Rwaya ni hadithi zinazotokana na sisi wenyewe, njozi za binadamu kuhusu maisha yake, pia ni mawazo anayo yaunganisha mwandishi kutokana na ujuzi alionao (Mlacha na madumulla 1991:1).

Wamitila, (2003), anasema riwaya ni kazi ya kinathari  au kubinilizi ambayo huwa na urefu wa kutosha. Msuko uliojengeka vizuri, wahusika wengi walioendelezwa kwa kina, yenye kuchukua nafasi / muda mwingi katika maandishi na kuhusisha mandhari maalumu.

Riwaya ya Kiswahili ni ile ambayo inafungamana na utamaduni wa jamii ya Kiswahili maana watunzi wengi wamekuwa wakiandaa kazi zao wakirejelea utamaduni na mila wanazozifuata au kuziamini.
Kuna wataalamu mbalimbali wamejaribu kuelezea kwa kina juu ya riwaya ya Kiswahili, ili kutupatia jibu au maana ya riwaya ya Kiswahili.
Mlacha na madumulla, (1991:10), wanasema la muhimu hapa ni kuzingatia kuwa tunapozungumzia riwaya ya Kiswahili tuna maanisha riwaya zilizoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Riwaya ya Kiswahili ni ile ambayo inafungamana na utamaduni wa jamii ya waswahili…………… Senkoro (2011), anaeleza kuwa riwaya zilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi ya kiutamaduni.

Mahundo na Balosidya ( 1976:62), wanasema riwaya ni kazi ya kubuni, ni hadithi ambayo hutungwa kufuatana na uwezo wa fanani. Kuibusha mambo kutokana na mazoea au mazingira yake.

Ukubwa wa riwaya, unaweza kuwa wa kurasa zozote zile kwani si idadi ya maneno au kurasa tu ambavyo vitatufanya tuiite hadithi fulani kuwa ni riwaya na nyingine kuwa hadithi fupi, zipo riwaya kana Nyota ya rehema (1981), yenye maneno zaidi ya 54,000, kiza katika nuru, (1988), amnayo ina maneno kama 93,000, vilevile kuna riwaya kama vile Bwana Myombokera na Bibi Bugonoka (1980), ambayo ndio riwaya ndefu kuliko zote hivi sasa na inamaneno zaidi ya 195,000 (Mlacha na Madumulla, 1991:1).

Riwaya haitambuliki kutokana na ugumu au urahisi wa hadithi hiyo kwani Ngona (1988) ambayo inaonekena ni tata kuliko Asali chungu (1977), bado ni riwaya. (Mlacha na Madumula, 1991:2)
Riwaya tupi kama vile Nagona inaweza kuonekena ngumu zaidi kuliko hata Bwana Myombokera na Bibi Bugonoka, kwani urahisi au ugumu wa hadithi hutegemeana na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na msomaji mwenyewe, ujuzi wake kuhusu maisha na lugha, uzoefu wake na mapenzi yake kuhusu hadithi.

 Vilevile inategemea ufudni wa mwandishi katika kuelezea hadithi yake na uhusiano kimawazo baina yake na wasomaji wanao tarajiwa n.k. (Mlacha na Madumulla, 1991:2).
Tukianza kuzungumzia historia ya riwaya ya Kiswahili ni nuhimu kuhihusisha sana na fasihi simulizi. Uhusiano huu sio wa kimuundo, ingawa muundo wa masimulizi ulichangia kwa kiasi fulani katika riwarya nyingi za mwanzo, lakini zaidi ni uhusiano uliotokana na uandikaji wa hadithi za Kiswahili.

Edward Steere alipokusanya na kuhariri hadithi alizozipata kutoka kwa wakazi hadithi alizozipata tutoka kwa wakazi wa Zanzibar unaweza kuwa ndio wakati wa kwanza kuangalia histori ya riwaya yetu ya Kiswahili (Mlacha na Madumulla, 1991:11).
Historia ya riwaya ulimwenguni haina muda mrefu sana hasa inapolinganishwa na historia ya tanzu nyingine za fasihi kama vile ushairi, tamthiliya ya fasihi simulizi (Mlacha na Madumulla, 1991:7).

 Historia ya riwaya ya Kiswahili nayo haikupishana sana na hali hiyo ya kutanguliwa na tanzu nyingine za fasihi ( Mlacha na Madumulla, 1991:7).
Historia ya riwaya ya Kiswahili imeangaliwa katika sura tofauti na wataalamu na watafiti mbalimbali (Mlacha na Madumulla, 1991:8).
TUKI, (2004:48), inasema chimbuko maana yake ni mwanzo au asili, tanzu za asili zinaonesha kuwa ndio zinachangia kwa kiasi kikubwa sana katika kuibia riwaya za Kiswahili.

Na yafuatayo ni mawazo ya wataalamu mbalimbali juu ya historia ya riwaya ya Kiswahili.

Wapo wataalamu waliyoiangalia historia ya riwaya ya Kiswahili pamoja na historia ya fasihi ya Kiswahili kama vile Rollins, 1993 (Mlacha na Madumulla, 1991:8).

Wapo wataalamu ambao wameangalia/ wamegusia uandishi wa hadithi (riwaya) za Kiswahili kama vile Balisidya (1976), senkora (1977), 1989), Ohly (1981), na mengine wengi ( Mlacha na Madumulla, 1991:8).

Baadhi wanaiangalia historia hiyo kuanzia mwishoni mwa karne ya kumi na tisa (19), ambao ni pamoja na Rajmund Ohly (1981), na wenzake wanaangalia historia ya riwaya ya Kiswahili wakati wa Edward Steere, ambaye mwaka 1870 alikusanya simulizi na mwenyeji wa Zanzibar na kuzihariri.

Hadithi hizi zilikusanywa na kuandikwa kwa lugha ya kingereza. Wataalamu hawa wanaiangalia historia ya riwaya kuanzia kwenye chanzo chake na vilevile kuanzia kwenye hatua za mwanzo katika maendeleo yake (Mlacha na Madumulla, 1991:8).

Wapo wataalamu wengine ambao wanaona kuwa historia ya riwaya ya Kiswahili ulianza robo ya kwanza ya karne ya 20 ambapo vitabu kama vile, mwaka katika minyororo (Mary Sehoza, 1921), viliandikwa.

 Mtaalamu mwingine aliyeungu mkono hoja hii ni Senkroro (1976), walichangia hoja hiyo wakiwa wametanguliza kitabu cha James Mbotela (1934), cha uhuru wa watumwa kuwa ndicho kilichoweza kuchukuliwa kama mwanzo wa historia ya riwaya ya Kiswahili (Mlacha na Madumulla, 1991:8).

Senkoro, (1976:75), anasema kuwa ……………………. Riwaya ya Kiswahili ndipo hasa ilipoanza wakati James Mbotela alipoandika uhuru wa watumwa.

Hii ndio ilikuwa riwaya ya kwanza ya Kiswahili nayo ilikuwa na mandhari ya hukuhuku Afrika Mashariki, wahusika walikuwa  waswahili, na mandhari yake yaliwahusu waswahili kwa jumla, waandishi mwenyewe alikuwa mswahili.
Wapo wataalamu wengine ambao wanadai kuwa historia ya riwaya ya Kiswahili imefunguliwa mlango na Shaaban Robert.

Wataalamu hao ni akina Elena Bertoricini (1983:85), Shegov (1976), na Rollins (1983) (Mlacha na Madumulla, 1991:9).

Hawa Rollins, (1983), Shegov, (1976) na Elena Bertoncini (1983:85), wanaichukulia historia ya riwaya ya Kiswahili katika hatua yake ya juu kimaendeleo na kuacha pengo kubwa ambalo ndilo hasa lililoweka msingi wa kukua kwa riwaya ya Kiswahili (Mlacha na Madumulla, 1991:9).

Kwa mtazamo wangu historia riwaya ilianza tangu karne ya kumi na nane kipindi ambacho Steer E. alipokuwa anakusanya hadithi fupifupi kwa wenyeji wa Zanzibar kwani hapa ndio ilikuwa hatua ya awali ya kuijua na kuiandika riwaya ya Kiswahili.
Baada ya kuangalia kwa kina historia ya riwaya ya kiswahili tangu kwenye chanzo chake ni vyema tukaingia kujadili maendeleo ya riwaya ya Kiswahili mpaka hapa ilipofika na ikiwezekana kubashiri ni wapi inapoelekea au itafika baada ya miongo mitatu au mine ijayo.

Kuna wataalamu mbalimbali wamejaribu kuelezea maendelo ya riwaya ya Kiswahili na katika mjadala huu  nitajaribu kuelezea wachache ili kuona maendeleo ya riwaya ya Kiswahili kwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Katika kuelezea riwaya ya Kiswahili, waingereza walitilia mkazo hadithi fupi na masimulizi mengine (Mlacha na Madumulla,1991:12).

Maendeleo ya riwaya ya Kiswahili yanameza kugawanyika katika vipindi tofauti tofauti kama ambavyo wataalamu mbalimbali wanaelezea na kujaribu kugawa kama ifuatavyo:-
Kipindi cha kwanza katika historia ya riwaya ya Kiswahili kinaishia mwaka 1910, kipindi cha pili (1910 – 1920), kipindi chabtatu mwaka 1929. (Mlacha na Madumulla, 1991:12).

Mwaka 1920 Heller A. B na wenzake walianzisha vijigazeti ambavyo viliandika hadithi tofauti. Hadithi hizi ziliweza kuwafikia wenyeji wachache ambao walikuwa na ujuzi wa kusoma (Mlacha na Madumulla 1991:12),
Wahariri wa magazeti walitoa hadithi katika magazeti kama vile mamboleo, walimwengu na mengine machache hadithi zilizotolewa ni Kama vile “kibaraka”, sultan zuwera”, Asha Binti Fulani, na nyingine nyingi. Hadithi hizi ziliwapa waandishi wenyeji nafasi ya kujitokeza katika uandishi na kujifunza kujieleza kifasihi na kifasaha. Mnamo mwaka 1921 hadithi kama vile mwaka katika minyororo, tuliyoyaona na tuliyofaya uingereza, viliandikwa na waandishi wenyeji wa mwanzo kama vile Sehoza na Kayamba (Mlacha na Madumulla 1991:12-13).

Kuundwa kwa kamati ya lugha ya Afrika mashariki mnamo mwaka 1929, kazi ya Kamati hii ilikuwa na nafasi kubwa sana katika kuendeleza lugha ya Kiswahili fasihi ya Kiswahili. Mmoja wa wanakamati hii alikuwa ni hayati Shaaban Robert, ambaye alikuwa ni mwanafasihi na mwandishi maarufu mno katika Afrika ya mashariki kwa kazi zake mbalimbali kama kusadikika (1951)  Adili na Nduguze (1952), utubora mkulima (1968), maisha yangu (1966), siku ya watenzi wote (1968), (Mlacha na  Madumulla, 1991:13).
Ripoti ya magavana, tukirejea katika historia kipindi hiki nchi za Afrika mashariki zilikuwa bado zinatawaliwa na mataifa ya kibepari, Tanganyika na Ujereumani Uganda na Kenya Uingereza wakati Zanzibar ili kuwa chini ya utawala wa Sultani, ambayo ilionesha umuhimu wa kuwa na Kiswahili katika shule na kuwa na Lugha sanifu ambayo ingetunika  katika kujieleza kifasaha na kifasihi ilikuwa ni ripoti muhimu katika maendeleo na hitoria ya riwaya ya Kiswahili (Mlacha na Madumulla 1991:13).

Kuanzishwa kama shirika la uchapishaji wa riwaya fupi za Kiswahili na kitabu cha mwanzo kilikuwa mwaka 1950 , kitabu kilichoitwa Mwarabu na binti yake.

Waandishi maarufu kama vile Shaaban Robert walijitokeza na kuandika (Mlacha na Madumulla, 1991:13).
 Shirika la uchapishaji vitbu la Afrika Mashariki (EACB) lilianzishwa mwaka 1948 ili kushughulikia uchapishaji wa vitabu shirika hilo lilipewa muhuri wa udhibiti wa maandishi, na kati ya 1948 na 1960 lilichapisha karibu vitabu 1000 kwa ajili ya shule na wasomaji wa kawaida kulikuwa na vitabu vya hadithi , hasa za kingano, hekaya na visa hapa ndipo Riwaya ya Kiswahili zilizopevuka zilianza kuchapisha miaka  kumi baadaye. Riwaya zilizoanza kupevuka kipindi hicho ni Farsy , kurwa na Doto (EACD 1960) na M.S Abdulla, Mzimu wa watu wa kale (EACB 1960) (Mulokozi 1996: 164).

Kazi za fasihi ya kizungu zilianza kutafsiriwa kwa Kiswahili kuanzia mwishoni mwa Karne ya 19, mfano wa kazi hizo ni C.Kingslay, mashujaa Hadith za wayunani 1889
Wakati wa ukoloni zilitafsiriwa  kazi nyingi zaidi za kigeni , mathalani, Banyan, J, Safaari za msafiri (Pilgrim’s progress) S.P.C.K, London 1925), Hekaya za Abunuwas (Msafii S. chiponde, Macmillan 1928) na kazi nyingine muhimu zilizofasiriwa ni baadhi ya tamthiriya za Willim shakespear kama Mfanya Biashara wa Venisi katika mtindo wa kinathari (Mulokazi 1996:164).

 Mwaka 1930, uandishi katika lugha ya Kiswahili ulihimizwa kwa njia ya mashindano ili tokana na agizo la kamati ya lugha ya Afrika mashariki kuanzisha mwaka 1929 na kutokana na mashindano hayo, riwaya ya kwanza ya  Kiswahili , Uhuru wa watumwa (James Mbotela 1885 – 1976), ilichapishwa mwaka 1934. Baadaye baadhi ya riwaya zilitoka kwa mfano M.S Abdulla, mzimu wa watu wa kale (EACB 1960), na faraji Katambala, simu ya kifo (EACB 1965), zilitokana na mashindano ya utumwa yaliyoendesha na kamati hiyo (Mulokazi 1996:164).

Miaka thelathini iliyofuata baada a uhuru wa watumwa inayoaminika kuwa ndio riwaya ya kwanza ya Kiswahili na James M, (1934). Ilitawaliwa na kazi za Shaaban Robert (1909 – 1962), Riwaya yake ya kwanza utubora Mkulima  (Nelson 1968) yasemekana ilitungwa mwaka 1946, lakini laikuchapisha hadi mwaka 1968. Riwaya iliyofuata ni kufikirika (OUP 1968) iliyoandikwa mwaka 1947 na kuchapisha mwaka  1967.

Riwaya ya tatu , kusadikika (Nerson 1951) ilichapisha mwaka 1951 na ya nne Adili na Nduguze (Macmillan, 1952) ilichapisha mwaka 1952. Riwaya yake ya Mwisho , siku ya watenzi wote  (Nelson 1968) iliandika kama 1960 – 62 na kuchapisha mwaka 1968 karibu riwaya zote za Shaaban  Robert  ziliathiriwa na ngano na hekaya, hasa katika muundo wake na uchoraji wa  wahusika (Karibu wahusika  wote ni bapa) (Muokozi 1996:164).

Kipindi cha miaka ya 1960  (1960’s) kwa afrika swala kuu lilikuwa ukombozi wa bara la Afrika na ujuzi wa jamii mpya baada ya uhuru . Hivyo palitokea riwaya za kisasa na kifalsafa zilizojadili maisha, utawala, na ujenzi wa jamii mpya. Riwaya za wakati huo zilijaribu kuelezea jamii katika mkondo wa ubinadamu usawa na ustawi mfano wa riwaya hizo Shaaban  Robert, Utubora Mkulima na siku ya watenzi wote (Mulokozi , 1996: 164).

Kuibuka kwa riwaya pendwa katika miaka 1960, hii ili changia maendeleo ya riwaya  ya Kiswahili kwani watu wengi walijotokeza kusoma kazi mbalimbali  ambazo zilipendwa na wasomaji miongoni mwa riwaya hizo ni Ms. Abdalla, mzimu wa watu wa Kale na Kisima cha Giningi (Evans,1968), (Mulokozi, 1996:165).

 Miaka ya 1970, riwaya Kiswahili imepevuka kupanuka zaidi mambo makuu yanayoipambanua riwaya ya kiswahili katika kipindi hiki ni:  (mulokozi 1996:165).

Kutokea kwa  watunzi wapya, vijana ambao wameipa uhai mpya riwaya baadhi yao ni E. kazilahabi (KZ 1944), Shafi Adam Shafi  (kuz 1940 ), M.S Mohamed (Kuz 1943), AJ. Safari kuz 1951), na B. Mpalal, (Kuz 1957).
Kuongezeka kwa  riwaya – pendwa ambako kuliambatana na kutokeza kwa wachapishaji waandishi kama John Simbamwene na E. Musiba ambao waliandika na kuchapisha riwaya zao wenyewe. Watunzi wa riwaya  pendwa katika kipindi hiki ni E. Musiba, Ben Mtobwa, J. Mkabarah, C. Merinyo, Mbunda  msokile (1950 – 1995), (Mulokozi, 1996:165).

Kujitokeza kwa riwaya inayohakiki jamii kwa undani, wengine wameiita  riwaya  ya uhakiki miongoni mwa waandishi hao ni shafi A. shafi, kasri ya mwinyi fuad (TAH 1978), na kuli  (TPH 1979), E. kazilahabi, Dunia uwanja  wa fujo (EACB 1975), G. Ruhumbika, Miradi Bubu ya wazalendo  (ERB 1992) . (Mulokozi, 1996:165).

Kuongezeka kwa riwaya za vijana na watoto, P. Shija mashujaa wa kaza kamba. (TPH 1978) na vijana Jasiri  (TPH 1980) M.M Mulokozi ngoma ya mianzi  (MPB 1990), Ngoma ya mianzi  (TPH 1991) na moto wa mianzi  (ECHOL 1995) (Mulokozi, 1996:165).

Kuzuka kwa riwaya ya wana kisomo, hii ni riwaya inayoandika mahususi kwa ajili ya wanakisomo wa madarasa ya elimu ya watu wazima na sifa za riwaya hiyo ni fupi, sahihi kimuundo, huwa na lugha rahisi, maudhui yake ni sahihi lakini ya kiwango cha watu wazima  (Mulokozi 1996:166).

Kuanzisha kwa taaluma ya uhakiki wa fasihi ya Kiswahili, taaluma hii ilianza kufundisha baada ya kuanzisha  kwa idara ya Kiswahili katika chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 1968 mnamo mwaka  1970, taaluma ya uhakiki imeenezwa mashuleni kote nchini , Taanzania na 1980 ilienezwa Kenya. Baadhi ya wahakiki mashariki ni kezilahabi 1976, Topan 1971, 1977; Sengo na Kiango 1973, 1994, TUKI 1983, Madumulla 1986; Mlacha 1990 , wamitila 1991 , msokile ni 1992 (Mulokozi 1996; 167).

Mwhisho katika mjadala nimejaribu kuelezea kwa kina historia na maendeleo ya Kiswahili katika  vipindi totauti bila kusahau chimbuko la  riwaya kwa ujumla. Tunaweza kuona kuwa riwaya ya Kiswahili imepita katika mikabala mingi mpaka katika karne hii ya 21.

MAREJEO
Abdalla, Ms. (1958), Mzimu wa watu wa kale . E.A.L.B Nairobi.
Mbunda M. (1992) , Kunga za fasihi na lugha, EPD , Dar es salaam
Mhando wa Balisidya  (1976) Fasihi na sanaa ya maonyesho .T.P.H Dar es salaam.
Mlacha S.A.K na Madumula J.S (1991), Riwaya ya Kiswahili, University press Dar es salaam
M.M , Mulokozi (1996) , utangulizi wa fasihi ya Kiswahili, chuo kikuu huria Dar es salaam
Ndungo C. W na wangani M (1991),Misingi ya nadharia za Kiswahili, universityof                                                                         Nairobi,Nairobi, Kenya.                                      
Robert, S.  (1952), Adili na nduguze, Macmillan Co. Nairobi
Robert,S. (1951) , Kusadikika, Nelson Nairobi
TUKI (1983), Miaka ya semina ya Kimataifa ya waandishi wa Kiswahili 2: Uandishi wa uchapishaji , TUKU, Dar es salaam.
Uganda, P.  (1959) ufunguo wenye Hazina, Evans Brothers.

masshele.blogspot.com

Share.

About Author

Leave A Reply