Sunday, August 18

FASIHI LINGANISHI NI TAALUMA INAYO JITEGEMEA , MJADALA

0


hujambo ndugu msomaji, je fasihi linganishi ni taaluma inayo jitegemea? Kwanza tutalii maana ya fasihi linganishi ndiposa tuangalie ikiwa fasihi linganishi unaweza kujitegemea pasi na kuhusisha na taaluma nyinginezo

Compbell (1926) Fasihi Linganishi ni taaluma inayochunguza uhusianao uliopo baina ya fasihi mbili au zaidi nje ya mipaka ya kitaifa kwa njia ya kulinganisha mfanano na msigano

Henry Remak (1971) anafasili Fasihi Linganishi kama uwanja wa kifasihi unaohusika na uchunguzi na mahusianao ya kifasihi nje ya mipaka ya nchi moja, pia kati ya fasihi na fani nyinginezo. Kwa maelezo haya ya Remak tunachoweza kusema ni kwamba Fasihi Linganishi haiishii kuangalia mahusino ya kifasihi peke yake bali huangalia mahusiano kati ya fasihi na fani nyinginezo zisizo za kifasihi.

Wamitila (2003) anaeleza kuwa fasihi linganishi inahusu uchambuzi wa maandishi ya wakati mmoja na aina moja na katika lugha mbalimbali kwa  nia ya kumiliki sifa zinazoyahusisha  kama athari, vyanzo, sifa zinazofanana na tofauti za kiutamaduni. Anaendelea kueleza kuwa inawezekana kufanya hivi kwa nia ya kuangalia matapo mbalimbali, maendeleo au hata nadharia za kiuhakiki. Fasihi ya namna hii iliweka misingi na juhudi za wanaisimu kuanza kuilinganisha lugha mbalimbali katika karne ya kumi na tisa.

Baada ya kuangalia fasili hizo je nikweli kuwa unaweza kuitenganisha fasihi linganishi na 

Historia, tafsiri, fiziolojia, utamaduni, anthropology, sayansi(uchunguzi), falsafa, nk ? 

Bila shaka jibu unalo sasa nakukaribisha katika mjadala

Info.masshele@gmail.com

Share.

About Author

Leave A Reply