Sunday, August 18

DHIMA ZA FASIHI LINGANISHI

0


Hujambo na karibu ndugu msomaji Leo tutaangalia kuhusu fasihi linganishi maana na dhima yake kijamii na kwa ujumla pia lakini kwanza embu tutalii maana ya fasihi linganishi

Compbell (1926) Fasihi Linganishi ni taaluma inayochunguza uhusianao uliopo baina ya fasihi mbili au zaidi nje ya mipaka ya kitaifa kwa njia ya kulinganisha mfanano na msigano

Henry Remak (1971) anafasili Fasihi Linganishi kama uwanja wa kifasihi unaohusika na uchunguzi na mahusianao ya kifasihi nje ya mipaka ya nchi moja, pia kati ya fasihi na fani nyinginezo. Kwa maelezo haya ya Remak tunachoweza kusema ni kwamba Fasihi Linganishi haiishii kuangalia mahusino ya kifasihi peke yake bali huangalia mahusiano kati ya fasihi na fani nyinginezo zisizo za kifasihi.

Wamitila (2003) anaeleza kuwa fasihi linganishi inahusu uchambuzi wa maandishi ya wakati mmoja na aina moja na katika lugha mbalimbali kwa  nia ya kumiliki sifa zinazoyahusisha  kama athari, vyanzo, sifa zinazofanana na tofauti za kiutamaduni. Anaendelea kueleza kuwa inawezekana kufanya hivi kwa nia ya kuangalia matapo mbalimbali, maendeleo au hata nadharia za kiuhakiki. Fasihi ya namna hii iliweka misingi na juhudi za wanaisimu kuanza kuilinganisha lugha mbalimbali katika karne ya kumi na tisa.

Baada ya kuangalia maana ya fasihi linganishi bila shaka sasa unaweza kueleza walau kidogo maana ya fasihi linganishi.

Sasa jibu swali lifuatalo je kwa kupitia fasihi linganishi tunaongezeka wapi katika utamaduni, siasa, kijamii, kifalsafa, kifasihi, kilugha, kiutafiti, na kimaarifa?

Itaendelea, info.masshele@gmail.com

Share.

About Author

Leave A Reply