Sunday, August 18

Nimepokea Kwa Furaha Sana Taarifa Za Dr . Slaa Kuwa Balozi Wetu Sweden..

0


Image may contain: 3 people, people smiling, people sitting

Ndugu zangu, 

Kupitia taarifa ya habari usiku huu nimezipokea taarifa kuwa Rais wa Jamhuri, Dr. John Magufuli amemtua Dr. Wilbroad Slaa kuwa Balozi wetu nchini Sweden.

Binafsi nimezipokea kwa furaha taarifa hizo. Rais wa Jamhuri ameonyesha umakini mkubwa kwenye teuzi zake ikiwamo hii ya Dr. Slaa kwenda Sweden.

Kimsingi Dr. Slaa ataiwakilisha nchi yetu Scandinavia yote ikiwamo nchi za Denmark, Finland na Norway hata Estland.

Binafsi nampongeza rafiki yangu na Mjamaa mwenzangu ( Social Democrat) Dr. Slaa kwa kupewa heshima hii kubwa kutuwakilisha kwenye nchi muhimu kwetu kihistoria na wakati huu kwenye mwelekeo wa diplomasia ya kiuchumi.

Karibu sana Sweden Dr Slaa! Valkommen Till Sverige!

PS: Pichani kamanda wangu huyo Manfred akiwa kwenye picha na Dr Slaa mwaka 2015 pale Mikumi. Mwaka huu yeye na pacha mwenzake Gustav wamehamia Sweden kimasomo, na sasa Dr. Slaa ndiye Balozi wao!Read More

Share.

Comments are closed.