Tuesday, August 20

Neno La Leo: Yesu Na Kipofu Yule Wa Yeriko..

0


 

Ndugu zangu,

Imeandikwa kwenye vitabu vitakatifu, Marko 10:46-52 
Yesu alipokuwa akiondoka Yeriko pamoja na Wanafunzi wake akatokea kipofu, jina lake Barti mayo. Kipofu huyu alikuwa ameketi kando kando ya njia, akiomba.

Kipofu yule alipomwona Yesu akapiga kelele;

“Yesu, Mwana wa Daudi, nionee huruma!”

Naye Yesu akasimama na akamwambia;

“Unataka nikusaidie nini?”

Ni nini basi tafsiri ya swali hili la Yesu kwa kipofu yule Barti Mayo?

Jibu:

Yesu hakutanguliza dhahania ( Speculation), kuwa kipofu yule alichotaka ni kuona. Kikubwa kuliko vyote kwa mwanadamu ni UPENDO. Yesu alionyesha upendo wa hali ya juu kwa kipofu yule kwa kuanza na kumwuliza; ” Unataka nikusaidie nini?”

Moja ya vilivyo na upendo mkubwa kwa mwanadamu kuvitenda kwa mwanadamu mwenzake ni kuuliza na baadae kusubiri jibu.

Ni hulka mbaya ya mwanadamu kutumia muda mwingi kujitanguliza mwenyewe. Kuzungumza juu ya yenye kumhusu na zaidi kujisifia. Hapo mwanadamu husahau kuuliza na kusikiliza.

Kama viongozi, mengine yanayotokea kwenye jamii yanatutaka tuanze na kuuliza, kisha tuyasikilize kwa kina majibu yanayotolewa na tunaowaongoza. Kisha, tuyafanyie kazi. Tusiyanyamazie.

Maana, Martin Luther alipata kutamka;

“Our lives begin to end the day we become silent about things that matter.”- Martin Luther King Jr.

Ni Neno La Leo.

Maggid.Read More

Share.

Comments are closed.