Sunday, August 18

Huyo Kamanda Wa Kwanza Kushoto Amepasua Mpaka Norway!

0


Image may contain: 2 people, people smiling, people standing, outdoor and nature

Image may contain: 3 people, people standing and outdoor

 

Ndugu zangu,

Kama wazazi zimetufikia habari njema kuwa kijana wetu Gustav ( Pichani kushoto) amefanikiwa kuvuka viunzi vyote na kuchaguliwa kujiunga na United World College ya nchini Norway kati shule 17 za aina hiyo duniani.

Nchi ya Sweden ina nafasi nane tu, Gustav alivuka hatua ya kwanza ya mchujo ya washiriki zaidi ya mia tatu. Akaingia kwenye 70 bora, kisha 20 bora na hatimaye kuingia kwenye 8 bora wanaohitajika.

Amepitia usaili mgumu na pia wameangalia aliyoyafanya nyuma. Ni hapa, faida ya mtoto kushiriki kazi za kujitolea kijamii zinampa pia pointi za ziada. Gustav kati ya kazi za kijamii alizozifanya akiwa Iringa, aliwaeleza juu ya kujitolea kwake kwenye kuwasaidia wahanga wa mafuriko kule Pawaga miaka kadhaa iliyopita kama inavyoonekana kwenye hiyo picha ya pili.

Nini tunachojifunza wazazi?

Tuwe wepesi wa kuwashirikisha na kuwahamasisha vijana wetu kufanya kazi za kujitolea, maana, maishani kuna mahala kuna watakaowauliza walifanya nini kusaidia jamii wakiwa vijana wadogo.

Kupita kwenye nane bora ina maana analipiwa na shule yake, gharama zote za kuishi na masomo, kasoro nauli ya kwenda na kurudi shuleni. Unaweza kusoma zaidi taarifa za shule hizi za UWC ikiwamo hiyo anayokwenda kusoma Gustav ifikapo Agosti mwaka huu. Angalia..https://en.wikipedia.org/wiki/UWC_Red_Cross_Nordic

Hongera Sana Gustav!!

Maggid.Read More

Share.

Comments are closed.