Thursday, August 22

Bongo Hapo Zamani: Kuna Mwingereza Aliyeandika Kitabu;

0


Ndugu zangu, 

Kuna tuliokua na kuiona Oysterbay ambayo hata ukipita inabidi uongee kwa sauti ya chini. Oysterbay ya miaka ya sabini ilikuwa na mandhari ya kuvutia sana ikiwemo usafi wa mazingira yake. Ilikuwa na miti mingi ikiwamo ya maua. 

Nyumba zake nyingi zilizungushiwa michongoma na ndani mtu uliweza kuona bustani za kuvutia. Mvumo wa upepo wa bahari, sauti za ndege na milio ya mbwa ilisikika hapa na pale.

Kuna kisa cha Mwingereza aliyekuja Tanzania baada ya miaka kumi ya Uhuru. Akafika Oysterbay alikopata kuishi. Akaiona Oysterbay nyingine kabisa.

Wakazi wapya, wengi watumishi Serikalini walibadilisha mazingira. Kuna waliokata miti na hata kuanzisha kilimo cha mbogamboga ikiwamo mahindi. Kuna waliofuga kuku, mbuzi, ng’ombe na kadhalika. Oysterbay haikupangwa kwa ufugaji wa ng’ombe.

Mwingereza yule akarudi kwao na kuandika kitabu; ‘ Bye Bye Oysterbay!’. 

Laiti Mwingereza yule angerudi tena baada ya miaka 50 ya Uhuru, basi, angeyakuta maghorofa na vioski na baa kwenye kona za Oysterbay. Angekutana na uchafu na hata harufu mbaya kwenye baadhi ya mitaa ya eneo hilo.

Mwingireza huyo angeandika kitabu kipya; ‘ R.I. P Oysterbay!’

Inahusu kutokuwa na nidhamu ya mipango miji yetu ambayo waliopanga waliangalia zaidi ya miaka 50 mbele.

Maggid.

 Read More

Share.

Comments are closed.